ULIMBWENDE: Maji ya mchele yana faida nyingi kwenye ngozi na nywele

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

MCHELE ukipikwa huitwa wali; chakula ambacho asilimia kubwa ya watu hupenda.

Maji ya mchele yana faida nyingi kwenye ngozi na nywele:

 • yanalainisha na kung’arisha nywele zako
 • yanajaza nywele kwa sababu yana amino acid
 • yanaimarisha nywele na kufungua vitundu vya ngozi (hair pores ) na kuzifanya nywele kukua vizuri
 • yana jukumu bora la kuondoa miwasho na mba kichwani

Kujaza nywele

Jinsi ya kuandaa

Andaa robo kilo ya mchele wa aina yoyote. Osha vizuri kisha weka kwenye sufuria yako safi.

Ongeza maji mengi au kadiria zaidi ya hapo mchele ulipoishia maana unafyonza maji sana.

Funika na uuchemshe kwenye sufuria uliyoinjika mekoni. Acha uchemke kwa dakika 10 hivi kwa moto wa wastani (usiive) au hadi uone mchele unaanza kulainika kwa mbali.

Epua na uache upoe kidogo kisha chuja na kitambaa au chujio safi.

Weka kwenye kopo maji uliyoyachuja na ufunike vizuri usiku kucha halafu asubuhi ongeza maji kikombe kimoja.

TANBIHI: Unaweza kutengeneza zaidi ukahifadhi kwenye friji kwa wiki mbili.

Safisha nywele zako na kisha zilowanishe na maji ya mchele kuanzia kwenye ngozi ya kichwa hadi kumaliza nywele zote halafu zifunike na kofia ya plastiki kwa dakika kumi kisha osha nywele zako na maji baridi bila shampoo au sabuni.

ULIMBWENDE: Unaweza kutumia tangawizi kukuza nywele zako

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

JE, wajua kuwa tangawizi ni nzuri sana kwa nywele zako?

Tangawizi ni nzuri kwa kuwa ina madini mengi na pia mafuta yanayohitajika kwa ajili ya kuzifanya nywele zako ziwe nyepesi na rahisi kuzitunza.

Kwa wale wote wanaosumbuliwa na mba na miwasho, tangawizi ni ‘dawa’ nzuri kwa kulinda ngozi yako kwa kuwa ni anti-fungal ya kiasili, anti-septic na pia anti-inflammatory inayozuia matatizo na maradhi yoyote yale ambayo yanaweza kushambulia ngozi yako.

Unapaswa kupaka tangawizi kwenye nywele yako angalau mara moja kwa mwezi.

Nywele zako zinahitaji kufanyiwa hivi ili ziwe na nzuri na za kupendeza; na kama wewe umekuwa ukisumbuliwa na mba kwa muda mrefu, jaribu na bila shaka utapata matokeo mazuri.

Namna ya kutumia tangawizi kwenye nywele

Toa maganda ya juu ya tangawizi.

Iponde halafu kamua maji yake.

Hayo maji yake unaweza kuyachanganya na asali au parachichi au Aloe vera.

Tangawizi isiwe nyingi; chukua kiasi kidogo tu.

Baada ya hapo, unapaka kuanzia chini kupanda juu na huku ukimasaji ngozi yako.

Halafu funika nywele zako kwa kitambaa kwa muda wa saa moja.

Baada ya hapo, osha ukitumia maji mengi.

Baada ya kuosha utapaka leave in conditioner.

Unaweza ukatumia tangawizi kuzitunza nywele zako

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

JE, wajua kuwa tangawizi ni nzuri sana kwa nywele zako?

Tangawizi ni nzuri kwa kuwa ina madini mengi na pia mafuta yanayohitajika kwa ajili ya kuzifanya nywele zako ziwe nyepesi na rahisi kuzitunza.

Kwa wale wote wanaosumbuliwa na mba na miwasho, tangawizi ni dawa nzuri kwa kulinda ngozi kwa kuwa ni anti-fungal ya kiasili, anti-septic na pia anti-inflammatory inayozuia magonjwa yoyote yale ambayo yanaweza kushambulia ngozi yako.

Unapaswa kupaka tangawizi kwenye nywele zako angalau mara moja kwa mwezi.

Nywele zako zinahitaji kufanyiwa hivi ili ziwe nzuri na za kupendeza.

Kama wewe umekuwa ukisumbuliwa na mba kwa muda mrefu, jaribu tangawizi na bila shaka utapata matokeo mazuri.

Namna ya kutumia tangawizi kwenye nywele

Toa maganda ya juu.

Iponde halafu kamua maji yake.

Hayo maji yake unaweza kuyachanganya na asali au parachichi au mshubiri.

Tangawizi isiwe nyingi; tumia kidogo tu.

Baada ya hapo unapaka kuanzia chini kupanda juu na huku ukimasaji ngozi yako.

Halafu funika nywele zako kwa kitambaa kwa muda wa saa moja.

Baada ya hapo osha kwa maji mengi.

Baada ya kuosha utapaka leave in conditioner.

‘Kusuka mabinti na kuwarembesha kucha ni riziki tosha’

Na SAMMY WAWERU

Ususi ni mojawapo ya gange inayoaminika kupaswa kufanywa na wanawake pekee, kwa kuwa ni kazi inayohusisha wateja wa jinsia ya kike.

Hata hivyo, dhana hiyo sasa imeonekana kupitwa na nyakati, vijana jinsia ya kiume wakiichangamkia na kuigeuza kuwa mtandao wa kuzimbua riziki.

Molo Market, soko lililoko katika kaunti ya Nakuru, saluni Jimmy Wa Cutex ina sifa za kipekee kutokana na umaarufu wake katika shughuli za kusuka na kurembesha wanawake.

James Wa Wanjiru ndiye mwasisi na mmiliki wa ‘karakana’ hiyo ya kurembesha kina dada, aliyoianzisha mwaka uliopita, 2019. Ikizingatiwa kuwa ni msusi wa jinsia ya kiume, wateja hufurika kupata huduma zake.

“Eneo hili wengi hawajaona wanaume wakisuka, ni jambo linalowavutia, hatua inayochangia kuimarisha huduma ninazotoa,” James anasema.

Ikiwa ni ndoto yake kuwekeza katika sekta ya biashara, kijana huyu anasema kufungua saluni hiyo ilikuwa mojawapo ya maazimio yake maishani. Ndoto hiyo haijaanza leo wala jana, ila miaka kadhaa iliyopita.

Kwa sababu ya ukosefu wa karo, James, 28, anasema alisoma hadi darasa la nane, ambapo alifanya mtihani wa kitaifa KCPE mwaka wa 2008. “Wazazi hawakuwa na uwezo kifedha, na nililazimika kutafuta vibarua vya hapa na pale kukithi riziki na kujiendeleza kimaisha,” anaelezea, akifichua kwamba alikita kambi Kericho ambapo aliajiriwa kuuza soseji na matunda.

James anaendelea kueleza kwamba iwapo kuna jambo lililomtia motisha, ni kuona mwajiri wake akipokea mapato ya mauzo aliyofanya mchana kutwa. “Japo mshahara ulikuwa duni, nilitamani sana wakati mmoja kumiliki biashara,” anasema.

Kijana huyu anasema alikuwa na mapenzi ya dhati katika safu ya sanaa, kupaka kucha za wanawake hina, rangi na kuzinakshisha. Kulingana na James, uchoraji ni kipaji alichojaaliwa na Mungu, ambapo akiwa shuleni anasema aliishia kuvurugana na walimu kwa kile anataja kama “kurembesha vitabu kwa kuchora vibonzo kwa wino”.

Ni kazi ya mikono, macho na kutumia bongo kuimarisha ubunifu na hatimaye aliiingilia. Katika harakati hizo, ususi ulianza kumvutia.

Mnamo 2017, kwa mtaji wa Sh50 pekee anazosema alitumia kununua kichana, alianza ususi tamba. “Kunakshisha kucha inaenda sambamba na ususi, hivyo basi nilijumuisha huduma hizo,” anadokeza.

Ni safari iliyokuwa na milima na mabonde, akisema changamoto kuu ilikuwa kutoza mteja nauli ili kumfikia. Aidha, alivumisha huduma zake kupitia mitandao ya kijamii, Facebook – Jimmy Wa Cutex ikiwa nembo maarufu kwa watumizi. “Baada ya kusuka wateja, nilipiga picha za staili na mitindo niliyofanya na kuzipakia mitandaoni zikiandamana na nambari za rununu,” anasema.

Jitihada hizo ndizo zilifanikisha James kufungua saluni yake eneo la Molo 2019, kwa mtaji wa Sh30, 000 alizoweka kama akiba kupitia huduma tamba. Kufikia mwezi Desemba, msusi huyu anasema kiwango cha mapato kilikuwa kimefika faida isiyopungua Sh2, 000 kwa siku.

Ni mjasirimali aliyebuni nafasi za ajira kwa vijana, na kufikia sasa ana wafanyakazi wanne. Licha ya kuwa alitamani kuwa mwandishi na mtangazaji wa habari ila karo ikakosekana kujiendeleza kimasomo, anajivunia kuwa katika sanaa ya ususi na urembeshaji wa wanawake, akifichua kwamba ameweza kuhudumia watangazaji tajika nchini.

“Ninashauri vijana wapalilie talanta walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu. Ajira za afisi ni haba, kupitia vipaji vyetu tunaweza kubuni kazi,” James anahimiza, akisema kuna vipaji wengi mno nchini na serikali inapaswa kuwapiga jeki na kuwahamasisha.

“Serikali ifanye hamasisho vijana watumie talanta walizojaaliwa kujiimarisha kimapato na kimaisha. Kikwazo kilichopo ni ukosefu wa fedha kati yao, hivyo basi iwapige jeki,” anaeleza msusi huyo.

Staili na miundo ya ususi anayofanya ni pamoja na braids, weave, retouch dreads, lines, kulainisha nywele, kuzipaka rangi, miongoni mwa zingine. Huduma zingine ni kama vile; Pedicure, manicure, cutex na gel polish.

Ususi na huduma zake, zinagharimu kati ya Sh100 – 2, 000.

Wakati wa mahojiano, James alisema janga la Covid – 19 limeathiri kwa kiasi kikuu biashara yake. Alisema kiwango cha wateja kimeshuka kwa asilimia 70.

“Watu (akimaanisha wateja) wanaogopa kusukwa kwa sababu hawajui nilisuka nani awali, kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya corona,” akasema, akiongeza kueleza kwamba amezingatia taratibu, vigezo na masharti ya wizara ya afya kuzuia maambukizi ya virusi hivi hatari.

Kilio chake kinawiana na cha Samuel Karanja, msusi tajika kaunti ya Nairobi, ambaye anasema amelazimika kufunga saluni yake. “Ninaifungua kupitia oda. Corona imeathiri utendakazi kwa kiasi kikuu,” analalamika.

ULIMBWENDE: Jinsi mwanamke anavyoweza kuzitunza nywele zake bila gharama kubwa

Na MISHI GONGO

AGHALABU kila mwanamke mwenye kujiamini hupenda kuwa na nywele za kupendeza na zilizo na afya tele.

Lakini hali mbalimbali zikiwemo mazingira, hali ya afya, lishe, familia na kadhalika huwafanya baadhi ya wanawake kuwa na nywele hafifu zisizokuwa na mvuto. Utawaona wanawake wakinyonyoka au kukatika kwa nywele, wabisi, nywele kuwa kavu mno au kukosa kukuwa.

Kufuatia gharama kubwa za kuhudumiwa na wataalamu ili kurekebisha matatizo hayo, baadhi ya wanawake wamezumbua njia za kiasilia kupambana na matatizo hayo.

Njia ya kwanza ni kutumia maji ya Aloe vera yaani mshubiri.

Mtumiaji anapaswa kuchukua jani la mshubiri kisha kulipasua na kuvuna maji au ute wake.

Ute huo unapaswa kupakwa kwenye ngozi kichwani. Ute huo huwa na uwezo wa kuzizimisha ngozi na kwa mtu aliye na wabisi hupata afueni na kuondokewa na kadhia ya kujikuna.

Aidha Aloe vera inaaminika kumiliki virutubisho kama vitamini A, E na C ambavyo vinasaidia katika kukua kwa nywele na kuzitunza kuzuia zisikatike au kunyonyoka.

Bidhaa nyingine ambayo inasifika katika utunzaji wa nywele ni yai.

Kuna baadhi ya watu ambao huchanganya yai na asali na kupaka nyweleni kisha kuziacha kwa muda wa nusu saa ili kuzipatia nywele zao afya, kuondoa wabisi, kuzikuza, kuzizuia zisikatike na kuzifanya ziwe na rangi ya kupendeza.

Parachichi pia hutumika na walimbwende katika utunzaji wa nywele kutokana na uwepo wake wa mafuta asilia. Waliowahi kutumia tunda hili, husema hukuza nywele maradufu.

Kutumia parachichi mrembo anatakiwa kufanya rojo kisha kupaka katika nywele zake kutoka kwa mashina hadi ncha. Zinapokolea anayetumia hupaswa kuzifunika kwa mfuko au kofia kwa muda wa dakika 20 kisha kuosha kwa maji baridi.

Tui zito la nazi nalo pia linasifika hasa na watu wa Pwani katika kutunza nywele. Mwanamke anapaswa kukuna nazi kisha kuchuja tui zito na kulipasha moto hadi liwe vuguvugu. Baadaye likishapoa kiasi, analipaka katika nywele zake kutoka kwa mashina hadi ncha huku akikanda kichwa chake taratibu kuruhusu mzunguko wa damu. Anapomaliza shughuli hiyo, anaosha kwa maji fufutende.

Tui la nazi linasifika kwa kukuza nywele, kuzuia kukatika, kuondoa wabisi, kuzifanya ziwe nyororo na kuzifanya ziwe na rangi nyeusi iliyopasha au iliyokoleza.

ULIMBWENDE: Jinsi ya kuhakikisha nywele zako zinakua haraka

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

KAMA wewe umeanza kukuza nywele na nywele zako hazikui haraka kama ulivyotegemea basi inawezekana hauzitunzi vizuri.

Nitakuelezea njia unazoweza kutumia kukuza nywele zako haraka na kukujulisha ni makosa gani ambayo yamkini umekuwa ukiyafanya yanayositisha ukuaji wa nywele zako.

Kosa la kwanza, ni kwamba watu wengi wananyoosha nywele zao mara kwa mara. Mtu akifanya hivi, ndiyo basi tena anakuwa anaziua nywele zake na zitaanza kukatika wakati wa kuchana au muda wowote. Basi inabidi upunguze kutumia vifaa kama hivi ili nywele zako zikue.

Pili, tunavyoziachia nywele na kusuka mtindo wa rasta, nywele za kawaida au kushonea ‘weave’ zinakubalika, ila ukizichana na kuzibana nywele basi hapo kuna uwezekano mkubwa kwamba zitaharibika au zitakatika.

Pia, kutokukata ncha baada ya muda, ncha zinaweza kuanza kuchanika na inabidi uzikate ili nywele zikue vizuri kwa sababu ncha huchangia kwenye kusitisha ukuaji wa nywele na kukata nywele zenyewe. Unaweza kukata ncha sentimita mbili baada ya miezi mitatu au minne.

Kutunza

Kwanza, inabidi uzisuke nywele zako mara kwa mara ili zisiharibike au zisikatike. Hivi utaweza hata kuzuia ncha zilizoharibika.

Kama hujisikii kusuka nywele au kushonea ‘weave’ basi unaweza kuzibana kwa juu au kuzifunga ukitumia kitambaa bora tu kiwe cha silk ili nywele zako zisiharibike (unaweza kukitumia hata wakati wa kulala).

Pili, inabidi upake mafuta kwenye kichwa chako mara kwa mara; hasa unapojisikia kama kichwa kimekauka au kama kinawasha. Mafuta mazuri kutumia kwa ajili ya ukuaji wa nywele ni mafuta ya nazi, castor oil, Moroccan, Jamaican au lavender. Unaweza pia kutumia mafuta mengine yoyote bora tu yasiwe ya mgando.

Pia, usizioshe nywele kwa kutumia shampoo mara kwa mara kwa sababu inaondoa mafuta kwenye kichwa na nywele zako.

Basi, inabidi uoshe nywele na conditioner kama unaona nywele zako sio chafu sana, ila kama unaona nywele zako ni chafu, basi osha ukitumia shampoo.

Itakuwa bora ukipaka mafuta kabla hujaosha nywele na uoshe nywele zako kila baada ya wiki moja na kama zinakatika, basi osha baada ya wiki mbili au tatu.

Vilevile ni muhimu kula vyakula vingi vyenye protini kama kuku, maharagwe au nyama yoyote inayokubalika.

ULIMBWENDE: Epuka makosa haya wakati wa kuosha nywele zako

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

AGHALABU kila mmoja wetu anawajibika kuziosha nywele.

Wengi wetu tumekuwa tukifanya makosa kadhaa wakati wa kuosha nywele. Baadhi yetu hatutumii muda wa kutosha kusugua ngozi ya kichwa, hatuoshi vizuri au pia hatutumii conditioner.

Yafuatayo ni makosa makubwa matano ambayo watu wengi huyafanya wakiwa wanaosha nywele.

Kutozitia nywele maji vizuri

Watu wengi hawaloweshi nywele zao vizuri kabla ya kupaka shampoo. Ni muhimu kulowesha kila unywele kwa maji kabla ya kupaka shampoo ili kutakata vizuri.

Kutumia shampoo nyingi sana au kidogo sana

Sote tunafahamu kwamba kitu chochote kikizidi kina madhara au hakitaleta matokeo mazuri. Tunatakiwa kutumia kila kitu kwa kiasi. Si kwa wingi sana na si kwa uchache sana.

Kutumia shampoo nyingi kunaweza kukufanya usiweze kuipata nywele na kuisafisha vizuri kutokana na kuzidiwa na povu jingi sana. Na kutumia shampoo kidogo kutafanya nywele zako zisitakate vizuri. Pima shampoo kiganjani mwako, kiasi cha wastani – kulingana na ukubwa na wingi wa nywele zako – kwa kutumia vidole paka shampoo kwenye nywele zako ulizozigawanya kwenye makundi manne. Paka kuanzia kwenye ngozi ya kichwa – scalp – hadi kwenye ncha ya nywele.

Kutotilia maanani zaidi ngozi ya kichwa

Kama umeshawahi ‘kufanyiwa shampoo‘ kitaalam katika saluni, bila shaka unajua ni muda kiasi gani huwa wanautumia kwenye ngozi ya kichwa.

Kusugua ngozi ya kichwa ni hatua ya msingi zaidi kwenye mchakato wa kuosha nywele.

Watu wengi hawatumii muda wa kutosha kusugua ngozi zao za kichwa. Tunatakiwa kusugua ngozi zetu za kichwa kwa angalau dakika tatu.

Bila kujali urefu au aina ya nywele zako, unachotakiwa ni kusugua ngozi yako ya kichwa. Na unatakiwa kufanya hivyo kwa kutumia vidole na sio kucha kwa muda usiopungua dakika tatu.

Kutokuosha na kurudia “rinse & repeat”

Ni muhimu sana kuosha nywele na kurudia. Na hii ni muhimu zaidi kwa wale wenye nywele ndefu.

Kama una nywele fupi au ndogo kabisa, si lazima kwako kuosha na kurudia.

Baada ya kuwa umesugua ngozi ya kichwa kwa dakika tatu, ni muda wa kuosha nywele. Ukishaosha inafuata hatua ya pili ya uoshaji wa nywele.

Unatumia shampoo kama kawaida. Kwenye hatua hii utaweka msisitizo zaidi kwenye nywele zenyewe kwakuwa tayari ngozi ya kichwa ulishashughulika nayo awali.

Mara hii weka msisitizo zaidi kwenye kuosha nywele zako na hakikisha hakuna nywele inayoachwa bila kupata shampoo kuanzia kwenye mzizi mpaka kwenye ncha.

Kutokutoa shampoo vizuri kwenye nywele.

Baada ya kurudia kuosha nywele kwa mara ya pili kinachofuata ni kutoa shampoo kwenye nywele.

Watu wengi hawatoi shampoo vizuri kwenye nywele, na hii huzifanya nywele kubaki na shampoo ambayo husababisha nywele kubaki na vitu vyeupe vyeupe na nywele pia kutosafishika vizuri.

Hivyo inasisitizwa kutumia muda na maji ya kutosha kutoa shampoo na kuhakikisha imetoka kabisa kwenye nywele ili nywele zako ziwe zimesafishika vizuri.

Wazee waficha mvi wasiuawe

Na WINNIE ATIENO

WAZEE eneo la Pwani wanalazimika kuvaa kofia kukuficha mvi wakihofia kuuawa. Pia wengi wameanza kupaka rangi nyeusi nywele zao wasije wakatambuliwa kuwa wana mvi.

Kwa muda sasa, magenge yamekuwa yakitekeleza mauaji ya kinyama ya wazee wenye mvi kwa kisingizio kuwa ni wachawi.

Kulingana na Mshirikishi wa Serikali Kuu eneo la Pwani, Bw John Elungata, wazee hao wameingiwa na hofu, ndiposa wameamua wawe wakivaa kofia ili kuficha nywele hizo, ambazo badala ya kuwa ishara ya busara zinawaweka kwenye hatari ya kuuawa.

Bw Elungata aliwaonya wakazi dhidi ya kuwauawa wazee hao kwa visingizio kuwa ni wachawi, lakini lengo kuu likiwa ni kuchukua mashamba yao.

“Wazee wanaficha nywele nyeupe kwa kuvaa kofia. Kuna sehemu fulani hapa ukionekana na nywele nyeupe uko hatarini,” akasema Bw Elungata.

Kulingana na mshirikishi huyo, wazee katika Kaunti ya Kilifi pia wameanza kupaka rangi nyeusi kwenye nywele zao ili wasiitwe wachawi na kuuawa.

“Tangu lini nywele nyeupe zikawa ishara ya uchawi? Hata mimi niko nazo na tunasema mvi ni upeo wa maisha ya mtu. Tusiwauwe wazee. Kwanza Kinango ndilo eneo hatari sana kwa wazee wenye mvi. Tunahitaji wazee ndiposa hata serikali inawalipa kila mwezi kwa kuwa ni mzee,” Bw Elungata alisisitiza.

Mwaka uliopita, zaidi ya wazee 60 katika kaunti za Kwale na Kilifi waliuawa kwa tuhuma za uchawi na masuala ya ardhi.

Mauaji hayo ya kiholela yalisababisha ujenzi wa sehemu ya kuokoa wazee ambao wanashukiwa kuwa wachawi wanakohifadhiwa katika sehemu ya Ganze, Kaunti ya Kilifi.

Zaidi ya wazee 87 wamewahi kutorokea makao hayo baada ya kushukiwa kuwa wachawi.

Kwa sasa kuna wazee tisa ambao wanahifadhiwa katika sehemu hiyo baada ya kuponea vifo.

Kulingana na mwenyekiti wa kituo hicho, Bw Emmanuel Katana, ukosefu wa chakula, maji ni baadhi ya changamoto zinazokumba makao hayo.

AFYA NA ULIMBWENDE: Vyakula vitakavyokuza nywele zako

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

KUWA na nywele zenye afya nzuri ni muhimu kwa wote bila kujali jinsia.

Hii ndiyo sababu baadhi ya watu huenda wakawa wanatumia dawa za aina mbalimbali za kuhakikisha nywele zao zinastawi na kuwa na mwonekano mzuri.

Lakini wengi wanaotumia dawa zinazotengenezwa kwa kemikali hujikuta katika wakati mgumu baada ya kuzitumia kwa muda kwani hukabiliwa na matatizo ya nywele kukatika na hata kupata madhara katika ngozi ya kichwa.

Njia bora na salama zaidi ya kustawisha nywele na kuzifanya ziwe na mvuto wa aina yake ni kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya ya nywele.

Yai

Nywele za binadamu zina protini.

Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa zina protini ya kutosha, na hilo hufanyika kupitia vyakula.

Protini ni nguzo kuu ya nywele za binadamu, na yai ni moja kati ya vyakula vyenye utajiri mkubwa wa protini.

Hakikisha unakula yai angalau mara tatu kwa wiki.

Mchicha

Nywele zinahitaji madini ya chuma ili ziweze kuwa katika hali nzuri kiafya. Kukosekana kwa madini ya chuma husababisha nywele kunyonyoka.

Mwili unapokosa madini ya chuma, hewa ya oksijeni na virutubisho hushindwa kufika vizuri kwenye mizizi ya nywele hivyo hufanya nywele kuwa dhaifu na zisizo na mwonekano mzuri.

Mboga za majani aina ya mchicha ni suluhisho, kwa kuwa zina madini ya chuma kwa wingi ambayo seli za nywele huhitaji.

Limau na machungwa

Mwili wa binadamu huhitaji vitamini C ambayo husaidia kuhuisha utendaji wa madini ya chuma. Hivyo, unapaswa kuongeza matunda ya jamii ya ‘citrus’ kama vile machungwa na limau. Pia, unaweza kutumia na asali pamoja.

Vitamini C husaidia katika ukuaji wa nywele, kusaidia usambaaji wa virutubisho na ukuaji wa haraka wa nywele.

Karoti

Karoti. Picha/ Maktaba

Ni muhimu sana kuhakikisha unakunywa juisi ya karoti kila siku kama unataka nywele zako zikue haraka zikiwa na mwonekano mzuri wenye afya.

Vitamini A inayopatikana kwenye karoti ni muhimu sana kwa ukuaji wa seli za nywele.

Karoti ina mafuta asili yanayofahamika kama ‘sebum’ na mizizi ambayo husaidia kukuza nywele kwa haraka.

Parachichi

Tunda aina ya parachichi lina kazi nyingi sana mwilini kama matunda mengine, lakini hili ni tunda la kipekee ambalo lina utajiri wa vitamini E ambayo husaidia mzunguko wa damu na katika hilo husaidia mfumo wa ukuaji wa nywele kwa haraka.

Tunda hili husaidia kuhuisha na kurekebisha mafuta na kiwango cha pH (inayosafisha kemikalii mwilini); vitu ambavyo kama vitazidi kwenye mwili vinaweza kusababisha kusimama kwa ukuaji wa nywele.

Kwa faida zaidi, vitamini E inayopatikana kwenye parachichi kwa wingi husaidia zaidi afya ya moyo wa binadamu na zaidi ngozi.

Hivi ni baadhi tu ya vyakula na matunda kwa ukuaji mzuri wa nywele zako.

ULIMBWENDE: Makosa ambayo baadhi ya watu hufanya wakati wa kuosha nywele

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

WENGI wetu tumekuwa tukifanya makosa kadhaa wakati wa kuosha nywele.

Baadhi yetu hatutumii muda wa kutosha kusugua ngozi ya kichwa, hatuoshi vizuri na baadhi pia hatutumii conditioner.

Kutolowesha nywele vizuri

Watu wengi hawaloweshi nywele zao vizuri kabla ya kupaka shampoo.

Ni muhimu kulowesha kila unywele kwa maji kabla ya kupaka shampoo.

Sote tunafahamu kwamba kitu chochote kikizidi kina madhara au hakitaleta matokeo mazuri. Tunatakiwa kutumia kila kitu kwa kiasi. Si kwa wingi sana na si kwa uchache sana. Hii ina maana kwamba kutumia shampoo nyingi kunaweza kukufanya usiweze kuipata nywele na kuisafisha vizuri kutokana na kuzidiwa na povu nyingi sana. Na kutumia shampoo kiasi kutafanya nywele zako zisitakate vizuri.

Pima shampoo kiganjani kwako, kiasi cha wastani kulingana na ukubwa na wingi wa nywele zako. Kwa kutumia vidole, paka shampoo kwenye nywele zako ulizozigawanya kwenye makundi manne. Paka kuanzia kwenye ngozi ya kichwa (scalp) kuja kwenye ncha ya nywele.

Watu wengi hawatumii muda wa kutosha kusugua ngozi ya kichwani. Tunatakiwa kusugua ngozi hizi kwa angalau dakika tatu.

Bila kujali urefu au aina ya nywele zako, unachotakiwa ni kusugua ngozi yako ya kichwa. Na unatakiwa kufanya hivyo kwa kutumia vidole na sio kucha kwa muda usiopungua dakika tatu.

Kutokuosha na kurudia (rinse & repeat)

Ni muhimu sana kuosha nywele na kurudia. Na hii ni muhimu zaidi kwa wale wenye nywele ndefu. Kama una nywele fupi au ndogo kabisa, si lazima kwako kuosha na kurudia. Baada ya kuwa umesugua ngozi ya kichwa kwa dakika tatu, ni muda wa kuosha nywele.

Ukishaosha, inafuata hatua ya pili ya uoshaji wa nywele. Unatumia shampoo kama kawaida.

Kwenye hatua hii utaweka msisitizo zaidi kwenye nywele zenyewe kwakuwa tayari ngozi ya kichwa ulishashughulika nayo kabla. Mara hii weka msisitizo zaidi kwenye kuosha nywele zako na hakikisha hakuna nywele inayoachwa bila kupata shampoo kuanzia kwenye mzizi mpaka kwenye ncha.

Kutokutoa shampoo vizuri kwenye nywele

Baada ya kurudia kuosha nywele kwa mara ya pili kinachofuata ni kutoa shampoo kwenye nywele.

Watu wengi hawatoi shampoo vizuri kwenye nywele, na hii huzifanya nywele kubaki na shampoo ambazo zinasababisha nywele kubaki na vitu vyeupe vyeupe na nywele pia kutosafishika vizuri.

Hivyo inasisitizwa kutumia muda na maji ya kutosha kutoa shampoo na kuhakikisha imetoka kabisa kwenye nywele ili nywele zako ziwe zimesafishika vizuri.

FUNGUKA: ‘Sipendi warembo wa nywele ndefu’

Na PAULINE ONGAJI

WANAUME wengi watakubaliana kwamba nywele ndefu huongeza urembo wa mwanamke.

Ni dhana iliyopo katika baadhi ya jamii na hata dini.

Huenda ni kutokana na sababu hii ndipo utapata kwamba sekta ya nywele ni ya thamani ya mabilioni ya pesa, kwani wanawake wengi wako tayari kufanya chochote kuafikia urembo huu unaohusishwa na nywele ndefu.

Ikiwa wewe ni mmoja wa hao mabinti basi huenda huna nafasi katika maisha ya Stanislaus, dume fulani lililokita kambi eneo la Mombasa.

Kwa Stanislaus hakuna binti anayeudhi kama yule aliye na nywele ndefu.

Lakini kabla ya kukusimulia zaidi hebu kwanza nikutambulishe kwa kaka huyu. Bwana huyu anafanya kazi na mojawapo ya kampuni zinazohusiana na utalii ambapo anahudumu kama meneja.

Mbali na taaluma yake ya kutamaniwa hasa kuambatana na kipato kikubwa inachomvunia, kaka huyu ameumbwa akaumbika ambapo anaakisi sifa zote ambazo humezewa mate na mabinti wengi.

Kifua chake ni kipana huku misuli ikichomoza kote.

Tumbo lake ni bapa, uso wake wa kupendeza, taya zilizobainika usoni, ngozi ya chokoleti, na mashavu ambayo kidogo yanakwaruza, kuashiria kuwa yeye ni dume ambalo bila shaka limekuwa likinyoa ndevu kwa miaka.

Sio hayo tu, Stanislaus, ni mojawapo ya madume wachache wasio na tabia ya kuchovya huku na kule hasa akiwa katika uhusiano.

Lakini usipumbazwe na sifa hizi. Kaka huyu amefanya iwe ngumu kwa mabinti kudumu naye katika uhusiano, kutokana na masharti yake hasa kuhusiana na nywele.

“Sipendi kamwe mabinti wa nywele ndefu. Ikiwa unataka kuwa wangu basi jiandae kunyoa nywele na kichwa chako kisalie kama uwanja.

Napenda mabinti walioonyoa vichwa kwani nataka wakati wa mahaba niweze kugusa kichwa chote pasi na vidole vyangu kusalia na mafuta, vumbi, au harufu inayotokana na jasho kwenye nywele ndefu.

Nataka mwanamke akioga aanze utosini hadi miguuni na kamwe siwezi kuvumilia harufu inayotoka kutoka baadhi ya vichwa vya mabinti hasa wanaopenda kusonga hizo nywele za kubandika. Upara unaashiria usafi kwani hakuna hatari ya chawa au wadudu wengine kupata hifadhi kwenye nywele.

Mbali na hayo, upara ni mbinu mwafaka ya kupunguza gharama. Siku hizi naskia kuna mabinti wanaotumia maelfu ya pesa kwa nywele za kubandika. Kwangu, pesa nyingi ambazo naweza kutumia kwa kicwa cha mwanamke ni Sh50. Play online pokies for free! Whether you’re a seasoned gambler or a newcomer, you are likely to find nonstop entertainment and endless opportunities to win with fun-filled promotions and lots of games in an online casino. To get access to the casino games you have to load your casino account and find where you can login to kings chance casino . You can find a good number of $5 deposit casinos in Australia.

Lakini haimaanishi kwamba ukiwa na nywele ndefu hauna fursa ya kuwa katika uhusiano nami. Fursa ipo, lakini uwe tayari kunyoa hizo nywele pindi tunapokubaliana rasmi kuwa katika uhusiano.”

Cha kushangaza ni kwamba kwa upande wake ameotesha shungi kichwani na anaamini kwamba yeye ni safi sana, na hivyo ana uwezo wa kudumisha usafi wa nywele, akilinganishwa na mabinti ambao anasema hawawezi kuaminika inapowadia katika masuala ya usafi wa kichwani.

ULIMBWENDE: Jinsi ambavyo unaweza kutunza nywele zako

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

WANAWAKE wengi wa Kiafrika husuka nywele zao kwa mitindo mbalimbali. Hii ina maana kwamba urembo wa kusuka nywele ni wa aina au jinsi mbalimbali.

Aina nyingine ni rahisi kutengeneza huku baadhi ikiwa ni ngumu ambapo inakuhitaji muda mrefu kuzitengeneza nywele.

Mitindo rahisi kama vile kuchana na kubana nywele huchukua muda usiozidi nusu saa wakati mitindo migumu kama rasta ndogo na nyembamba ikiweza hata kuchukua muda wa saa 5 hadi 8 kama unashughulikiwa na msusi mmoja.

Bei ya usukaji pia hutofautiana kulingana na ugumu wa mtindo na muda unaotumika.

Kunyoa kipara

Wapo wanawake wengi wanautumia mtindo huu wa kunyoa na wanapendeza.

Nywele fupi za kuchana au kusuka

Mtindo huu ni rahisi na pia unaweza kufanya mwenyewe nyumbani na ni wa haraka na hauhitaji pesa.

Nywele ndefu za kubana

Mtindo mwingine rahisi ni kuchana na kubana katika namna tofauti. Unaweza ukatumia vibanio vya nywele au ukazifunga kwa kitambaa.

Nywele zinatakiwa kupumzika kidogo baada ya kusukwa katika mitindo ya kubana sana.

Selfie ya Margaret Maina akiwa amezichana nywele zake. Picha/ Margaret Maina

Kutengeneza nywele

Mitindo hii ni migumu, huchukua muda mrefu na hivyo ina bei za juu kusuka.

1. Rasta za bandia

Mtindo huu hukuhitaji kutumia nywele bandia kusuka na ni mzuri na hufanya wanawake wengi wawe wa kupendeza.

2. Rasta za asili

Hizi, mrembo hahitaji kutumia nywele za kuongeza. Nywele asili husokotwa katika mafungu madogomadogo.

3. Laini (cornrows)

Ni mtindo maarufu na unapendwa na wanawake wengi – wa mashinani na wa mijini.

Tazama picha hizi:

Selfie ya Margaret Maina akiwa ametengeneza nywele zake nadhifu. Picha/ Margaret Maina
Margaret Maina akiwa ametengeneza nywele zake. Picha/ Hisani

Chagua mtindo utakaokufaa

Kuna mitindo mingi ya kusuka nywele, mingine ni rahisi na inahitaji muda mfupi wakati mingine ni migumu na inahitaji muda mrefu na ni ya gharama kubwa.

Ukiwa na muda mfupi wa kujiandaa utahitaji mtindo rahisi.

Pia mtindo utakaouchagua ama uwe ni mtindo wa ofisini au kama ni kwa ajili ya safari, unaweza ukatofautiana na ule wa kutengeneza kwa ajili ya sherehe au shughuli nyingine ya kijamii.

REKODI YA GUINNESS: Hajanyoa nywele kwa miaka 33 ili apate umaarufu

Na CHARLES WANYORO

MWANAUME ambaye hajanyoa nywele zake kwa muda wa miaka 33 yuko mbioni kuvunja rekodi kuwa mtu aliye na nywele ndefu zaidi ndefu zaidi nchini Kenya.

William Kaimenyi Rimberia, 59, mkazi wa kijiji cha Kambakia, Kaunti ya Meru aliacha kunyoa nywele na ndevu zake kama njia mojawapo ya kuunga mkono harakati za kupigania mfumo wa vyama vingi nchini. Mashungi yake ya nywele na ndevu sasa yamekuwa magumu na imara na yamefikia urefu wa mita moja.

Baada ya kufutiliwa mbali kwa kifungu cha sheria 2(a) kilichopiga marufuku mfumo wa vyama vingi mnamo Desemba 1991, Bw Kaimenyi aliamua kuendelea kutonyoa nywele zake na ndevu.

Anasema kuwa nywele ndefu, ambazo kwa kawaida huhusishwa na mashujaa wa Maumau, humfanya kuwa na na ujasiri wa kuendelea kupigania haki mbalimbali za kibinadamu.

“Lengo langu lilikuwa kunyoa baada ya mfumo wa vyama vingi kuhalalishwa. Baadaye niliamua kuendelea kukuza nywele na ndevu kama ishara ya ukombozi wa pili,” akasema.

Bw Kaimenyi ambaye ni mwanachama wa baraza la wazee wa jamii ya Wameru la Njuri Ncheke, amekuwa akipigania haki za wajane na watu wengine wanaodhulumiwa kutoka kijiji kimoja hadi kingine.

“Watu wengi wanakumbana na dhuluma mbalimbali hata leo. Kwa mfanoninafuatilia kesi ya mjane ambaye shamba lake lilinyakuliwa na kanisa mjini Maua. Mjane huyo alipata agizo la mahakama la kutaka kanisa hilo libomolewe mnamo 2014 lakini kufikia sasa hakuna hatua ambayo imechukuliwa,” akasema.

Licha ya kuwa mwanaharakati, Bw Kaimenyi anasema kuwa kufikia sasa hajapata fursa ya kuanzisha familia yake mwenyewe. Alisema nywele zake ndefu ni kivutio kikuu kwa wakazi wa eneo hilo ambao husimama na kumpiga picha wanapokutana naye.

Miaka michache iliyopita watu wenye nywele ndefu walihusishwa na kundi haramu la Mungiki. Lakini Bw Kaimenyi anasema kuwa hajawahi kuhangaishwa na yeyote kwa ‘kufuga’ nywele ndefu.

“Watu hunisimamisha njiani na kuanza kutamani nywele zangu. Kuna wakati nilienda katika Mahakama ya Juu kushughulikia kesi fulani na kila nilipopita watu walibaki na mshangao.

“Nywele zangu ni kivutio kikubwa kwa watu na ninafurahia kuwa nazo na wala haziniumizi ninapolala usiku,” akasema Bw Kaimenyi.

ULIMBWENDE: Tumia mbinu hii ya vitunguu maji kutunza nywele

Na MARGARET MAINA

MTU na hasa mwanamke anayetambua umuhimu wa mwonekano mzuri hutamani kuwa na nywele nzuri za kutosha na zenye afya yake ya asili. Tatizo la kupotea kwa nywele au upara (wengine hupenda hali hii) limekuwepo tangu awali. Kipara kinaweza kuja kwa sababu za kimaumbile za kawaida.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kupotea kwa nywele kama vile:

 • Sababu za kimazingira
 • Kuzeeka
 • Msongo wa mawazo (stress)
 • Kuvuta sigara kupita kiasi
 • Lishe duni
 • Homoni kutokuwa sawa
 • Kurithi vinasaba
 • Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa
 • Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele
 • Baadhi ya dawa za hospitali
 • Matatizo katika kinga ya mwili
 • Upungufu wa madini chuma, na
 • Magonjwa mengine sugu

Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binadamu kwani hutibu magonjwa mengi kama kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi, koo, figo, na pia kina virutubisho vingi vya vitamini C.

Kitunguu hiki huwa na salfa (sulphur) ambayo husaidia kutengeneza tishu za ‘collagen’ katika mwili ambapo huipa nywele na ngozi nuru ya aina yake.

Hivyo naweza kusema kuwa juisi ya kitunguu maji husaidia kukuza nywele na kwa wale wenye nywele za kukatika, kupaka kitunguu maji mara kwa mara kunaweza kusaidia kupambana na tatizo hilo.

Jinsi ya kuandaa

 • Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemea na na ukubwa wa kitunguu chenyewe
 • Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye
 • Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga
 • Saga kwenye blenda au uvitwange kwenye kinu.
 • Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi.
 • Vichuje vizuri ili upate majimaji. Hakikisha kwamba huongezi maji kwa hivi vitunguu.

Jinsi ya kupaka

Nywele sio lazima ziwe safi maana unapaswa kuziosha baada ya kupaka maji ya vitunguu.

 • Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka kichwa kizima.
 • Baada ya kupaka unapaswa kuvaa kofia ya plastiki na kitambaa kichwani ili uweze kupata joto.
 • Ukae hivyo kwa muda wa saa 4 – 5
 • Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako.

Hitimisho

Ni vyema kufanya shughuli hii ya kupaka vitunguu angalau mara mbili kwa mwezi.

Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza kuongezea asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.

Kwa matokeo mazuri ya kukuza na kutunza nywele zako, tumia vitunguu vidogo kufanya jinsi nilivyoeleza hapo juu.

VITUKO UGHAIBUNI: Mwanamume huyu hulipa Sh292,000 kunyolewa

Na MASHIRIKA na VALENTINE OBARA

NEW YORK, AMERIKA

BWANYENYE aliye raia wa Canada amefichua hutumia dola 2,920 (Sh292,000) kila mwaka kunyoa nywele.

Kevin O’Leary, 63, ambaye ni mashuhuri kwa ukwasi wake unaokadiriwa kuwa wenye thamani ya dola milioni 400 (Sh40 bilioni) na kushiriki kama mmoja wa majaji kwenye kipindi cha ‘Shark Tank’, alisema yeye huchukulia kwa umuhimu mkubwa nywele za kuvutia, hata ingawa ni kihara.

Kwenye mahojiano na shirika la habari la CNBC lililo Amerika, bwanyenye huyo alifichua huwa ananyolewa baada ya kila siku kumi, na hutumia dola 80 (Sh8,000) kila anaponyolewa.

“Mimi huwekeza katika hitaji la kuwa mtu wa kuvutia kila mara na huwa nafanya hivi kwa kuvaa nguo za kuvutia, viatu vizuri sana na kunyoa nywela kila baada ya siku kumi,” akasema.

Hata hivyo, aliongeza kuwa hapendi kunyoa kipara ambayo ni mtindo unaopendwa sana na wanaume wenye vihara.

“Sina nywele nyingi kwa hivyo huwa nataka kuwa na uhusiano na kila unywele kichwani mwangu. Watu huniuliza mbona nisinyoe nywele zote niwe kipara. Sipendi mtindo huo. Ninapenda mtindo huu. Nadhani navutia mno,” akasema.

Mama akiona kuokota nywele katika kinyozi

Na CORNELIUS MUTISYA

ITHAENI, MACHAKOS

Kwa Muhtasari:

 • Mwenye kinyozi aliwahudumia wateja wake na akafagia nywele. Hakujua kwamba kulikuwa na mama aliyekuwa akimtegea amalize kuzifagia.
 • Mwenye kinyozi alipoondoka, mama huyo alifika na akaanza kuziokota nywele hizo na kuzipakia kwa kikapu
 • Watu walifurika mara moja na wakaanza kumtandika mama huyo wakimtuhumu kuwa mchawi

MAMA wa umri wa makamo, alipokezwa kichapo cha mbwa koko na wakazi wa eneo hili walipofumaniwa nje ya kinyozi akiokota nywele za watu na kuzipakia katika kikapu. Wakazi walishuku alikuwa akitaka kwenda kutekeleza vituko vya ushirikina.

Kulingana na mdaku wetu, mwenye kinyozi aliwahudumia wateja wake na akafagia nywele hadi nje ili asubuhi wahudumu wa serikali ya kaunti waje kuzichukua na kuzipeleka kuzitupa kwenye jaa la takataka. Hakujua kwamba kulikuwa na mama aliyekuwa akimtegea amalize kuzifagia.

”Mhudumu wa kinyozi alifagia nywele na kuziacha nje ya mlango na akaondoka’’ akasema mdokezi.

 

Kuzitia kikapuni

Inasemekana kwamba, mwenye kinyozi alipoondoka, mama huyo alifika na akaanza kuziokota nywele hizo na kuzipakia kwa kikapu kilichochakaa. Hata hivyo, ni wakati alipokuwa akiendelea na shughuli hiyo, walinzi wawili walipomuona na wakamshuku.

Waliamua kumkabili na kumuuliza sababu ya kukusanya nywele hizo.

“Mama aliwaambia mabawabu hao alidhamiria kutengeneza gondoro na nywele hizo. Hata hivyo, jitihada zake za kujitetea ziliambulia patupu na walinzi hao wakapuliza firimbi’’ alisema mdokezi.

 

Mchawi

“Twaarifiwa kwamba, watu walifurika hapo mara moja na wakaanza kumtandika mama huyo wakimtuhumu kuwa mchawi. Alipokezwa kichapo cha mbwa koko nusura aone vimulimuli na akaokolewa na maafisa wa usalama kabla ya kutiwa moto. Wakazi walimlaumu mama huyo kwa kuwaroga akitumia nywele na vipande vya nguo zao,’’ alisema mdaku wetu.

Duru zaarifu kuwa wakazi walitaka mama huyo asukumwe seli lakini akaachiliwa kwa kukosekana kwa ushahidi wa kumhusisha na ushirikina.