• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Risala za heri na sifa tele Kibaki akigonga 90

Risala za heri na sifa tele Kibaki akigonga 90

Na WANDERI KAMAU

RAIS Uhuru Kenyatta jana aliwaongoza Wakenya kumpongeza Rais Mstaafu Mwai Kibaki na kumtakia maisha marefu, baada ya kufikisha umri wa miaka 90.

Mzee Kibaki alihudumu kama rais kati ya 2002 na 2013, ambapo alisifiwa kuchangia pakubwa kwa ukuaji wa uchumi.

Pia anakumbukwa kwa kuanzisha elimu msingi bila malipo.

“Tunakutakia neema ya Mungu unaposherehekea kufikisha miaka 90 tangu kuzaliwa kwako, Bw Kibaki,” ikaeleza taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Nairobi.

Viongozi wengine waliomtumia jumbe za pongezi ni Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka (Wiper), Waziri wa Utalii Najib Balala, Gavana Wycliffe Oparanya (Kakamega) kati ya viongozi wengine.

“Pongezi Bw Kibaki. Sifa yako itadumu daima,” akasema Dkt Ruto.

Bw Musyoka alimtaja Mzee Kibaki kuwa miongoni mwa viongozi bora zaidi ambao washawahi kuiongoza Kenya.

Bw Kibaki alizaliwa Novemba 15, 1931.

  • Tags

You can share this post!

Vita Ethiopia vyatishia hali ya Kenya

Ruto awasuta wanaotaka ajiuzulu

T L