• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Samaki azua hofu, akikuuma huonani na mke miezi 6

Samaki azua hofu, akikuuma huonani na mke miezi 6

Na KALUME KAZUNGU

WANAUME katika Kaunti ya Lamu wamekuwa wakiishi kwa uwoga wa samaki ambaye ni tisho kubwa kwa maisha yao ya kifamilia.

Samaki huyo aina ya taa ni mkubwa na mwenye umbo bapa na mkia mrefu ambao ncha yake ina maumbile kama ukucha unaoaminika kuwa na sumu kali.

Wakazi wa Lamu wanaamini anayedungwa na taa hastahili kushiriki mapenzi na mkewe kwa karibu miezi sita wakati akiuguza kidonda.

Mzee wa kisiwa cha Kizingitini, Bw Khaldun Vae, aliambia Taifa Leo kwamba imani hiyo imekita mizizi tangu jadi vijijini mwao kiasi kwamba baadhi ya ndoa zimekuwa zikikumbwa na matatizo punde waume wanapoujeruhiwa na samaki huyo.

“Tangu enzi za mababu zetu, huwezi kudungwa na mwiba wa taa na kabla hujapona unakimbilia kulala na mkeo. Huko ni kujichimbia kaburi,” akasema Bw Vae.

You can share this post!

WANTO WARUI: Migomo shuleni ichunguzwe vilivyo kubaini...

Miguna Miguna adai serikali imemzuia kurejea nchini

T L