• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Samidoh adai alitaka kuwa wakili, akifichua alama zake za KCPE

Samidoh adai alitaka kuwa wakili, akifichua alama zake za KCPE

NA MERCY KOSKEI

MSANII Samuel Muchoki Ndirangu almaarufu Samidoh amewaacha mashabiki wake vinywa wazi kufuatia chapisho la cheti chake cha mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE).

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Samidoh alichapisha mnamo Jumamosi Septemba 16, 2023 picha ya cheti chake cha KCPE iliyofichua alikamilisha masomo ya shule ya msingi 2004.

Mwanamuziki huyo alidokeza kwamba alitaka kuwa wakili, lakini katika shule ya maisha, hatima mara nyingi hubadilisha mtazamo wa mtu.

Baba huyo wa watoto watano, alishangaza watumizi wa mitandao alipofichua kwamba aliorodheshwa wa kwanza kufanya KCPE (Index one).

“Huyo index number one wa kwenu anafanyanga nini siku hizi, nilitaka kuwa wakili lakini mimi huyo one man guitar AKA singing police man,” alitania.

Samidoh ambaye pia askari wa kikosi tawala (AP), huimba nyimbo za Mugithi.

Hutumia gitaa kutumbuiza.

Wanamitandao walipotaka kujua alama alizopata katika Hisabati, mwanamuziki huyo aliandika: “Hehe si mko curious mimi ni mwalimu wa Maths tu hatukua tunaskizana sana otherwise, sikuelewana na mwalimu wangu wa Hisabati vinginevyo.”

Kulingana na cheti hicho, somo la Kingereza alipata B+, Kiswahili A-, Hesabu C+, Sayansi A, Jiografia, Historia na Somo la Dini B+.

Wengi walifurika kwenye safu ya maoni, wakitoa hisia tofauti.

Terence creative aliuliza: “Wapi mwalimu wa Math?”

Sammy Ondimu Ngare, askari mwenza, alimdadidisi: “Nataka Kuona CRE ulikuwa na ngapi…Bado unataka kuwa lawyer ama tuachie hapo?”

“Na Mungu akakubariki na wakili Karen. Aliona wewe uwe mtekelezaji sheria,” Asher Omondi aliandika.

Samidoh amekuwa kwenye mahusiano haramu na Seneta Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili.

Aliyekuwa mkewe, Edday Nderitu alimtema kufuatia uhusiano wake na mwanasiasa huyo wa chama cha UDA.

Aidha, Edday alihamia Amerika na wanawe watatu.

 

  • Tags

You can share this post!

Magaidi wawili wa Al-Shabaab wauawa na maafisa wa KDF...

Maina Njenga ‘atekwa nyara’

T L