• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:10 PM
Sayari 5 kuonekana angani Jumanne jioni

Sayari 5 kuonekana angani Jumanne jioni

NA MASHIRIKA

SAYARI tano zitaonekana kwa tukio la kipekee mnamo Jumanne jioni ambapo zitakuwa zimejipanga kwa safu ya kuvutia.

Sayari za Zaibaki (Mercury), Zuhura (Venus), Mirihi (Mars), Jupita, na Kausi (Uranus) zitaonekana muda mfupi baada ya jua kuzama kesho Machi 28 zikiwa zimejipanga kwa safu ya kupendeza.

Nchini Uingereza, Zuhura na Jupita ndizo sayari zitakazoonekana vizuri, lakini Zaibaki, Kausi na Mirihi hazitaonekana vizuri kwa mujibu wa Wanasayansi.

Prof Beth Biller wa Chuo Kikuu cha Edinburgh amesema watu walio mjini huenda wasipate fursa nzuri kuziona sayari kwenye safu.

Ameshauri wanaotaka kujionea vizuri, waende maeneo ya mashambani ambako ni rahisi kutazama juu angani bila kutatizwa na majengo marefu.

“Miji mingi huwa na majengo marefu yanayofanya iwe vigumu kwa watu wengi kujionea sayari,” amesema Prof Biller.

Ameongeza kwamba ni kawaida sayari tatu kuonekana zimepangika kwa safu, lakini ni nadra kwa sayari tano kujipanga kwa safu.

Hata hivyo, sayari tano zimewahi kujipanga kwa safu moja mwaka 2022, mwaka 2020 na mwaka 2016.

  • Tags

You can share this post!

Vyakula vya Iftar vinavyoenziwa Lamu

Wahamiaji 19 wafa maji wakielekea Italia

T L