• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 2:07 PM
Wario na Soi watozwa faini ya Sh109Milioni ama kifungo cha miaka 20 katika sakata ya Rio

Wario na Soi watozwa faini ya Sh109Milioni ama kifungo cha miaka 20 katika sakata ya Rio

Na RICHARD MUNGUTI

WAZIRI wa zamani wa michezo na jinsia Bw Hassan Wario pamoja na afisa aliyeongoza timu iliyowakilisha Kenya katika michezo ya Olimpik ya Rio De Janeiro, Brazil 2016 Bw Stephen arap Soi Alhamisi walioshtakiwa katika kashfa ya ufujaji pesa za wanamichezo jana walitozwa faini ya jumla ya Sh109,165,126.

Hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Bi Elizabeth Juma alimtoza Bw Wario faini ya Sh3.6milioni kwa matumizi mabaya ya mamlaka.Akishindwa kuilipa atatumikia kifungo cha miaka sita gerezani.

Wario alilipa faini hiyo mwendo was saa 11 alasiri na kuachiliwa kwenda nyumbani..Naye Bw Soi alitozwa faini ya Sh105,565,126 kwa ufujaji wa pesa za umma.Akishindwa kulipa faini hiyo Bw Soi atatumikia kifungo cha miaka 14 gerezani.

Punde tu hakimu alipopitisha  hukumu hiyo watu wa familia ya Bw Wario walimlipia faini hiyo kisha akaachiliwa huru.Kwa raha Bw Wario “aliinua mikono miwili na kusema hatimaye niko huru.”

Lakini Bw Soi hakuweza kulipa faini hiyo.Alipelekwa gereza la Viwandani.Wakili wake Bosek Kimutai alieleza mahakama atakata rufaa kupinga adhabu hiyo akisema mshtakiwa huyo “hakufaidi kutokana na pesa hizo serikali ilikuwa imetoa kugharamia marupurupu ya wanamichezo aliosema walipeperusha bendera yah ii Brazil walikozoa medali 13.”

Wario akiwa na mkewe kortini baada ya kutozwa faini ya Sh3.6milioni ama atumike kifungo cha miaka sita kwa matumizi mabaya ya pesa za umma…PICHA/RICHARD MUNGUTI

Kenya ilizoa jumla ya medali 13- sita za dhahabu, sita za fedha na moja ya shaba.Nchi hii ilikuwa nambari moja barani Afrika na nambari 15 ulimwenguni.Hata hivyo hakimu alisema sifa ya nchi hii iliharibika kashfa hiyo iliporipotiwa na vyombo vya habari.

Bi Juma alisema Bw Wario alitakiwa kusimamia vyema matumizi ya pesa zilizotengewa zoezi hilo la michezo.Bi Juma alisema Bw Soi alikuwa ametengeneza bajeti ya Sh583milioni kwa ajili ya michezo hiyo ya Olimpik.

Serikali ya Kenya ilikuwa igharamie Sh500milioni na kamati ya kimataifa ya olimpik (IOC) ighramie Sh83milioni.“Bw Soi alitayarisha bajeti hiyo ya karibu Sh600milioni akiwa na nia ya kuifuja nchi hii,” alisema Bi Juma.

Mahakama ilisema pesa hizo hazikuwafaidi wanamichezo waliopeperusha bendera ya nchi hii wakati wa michezo ambapo walipambana kufa kupona nchi hii ing’are.“Baada ya bajeti hii kutayarishwa Bw Wario aliwajumuisha watu ambao hawakustahili kusafiri na kuwanufaisha kwa njia isiyo halali,” alisema hakimu.

Alisema bajeti hii ya Sh600milioni ilikuwa kubwa na pesa zilizotumiwa vibaya zingelitumika katika miradi mingine ya kuinua hali ya maisha ya walipa ushuru.Akimtetea Bw Wario , wakili Rodgers Sagana aliiomba mahakama imwonee huruma mshtakiwa kwa vile ni mkosaji wa mara ya kwanza.

“Mshtakiwa alitimuliwa kazi ya uwaziri na kupokonywa wadhifa wa Balozi aliokuwa ameteuliwa punde tu sakata hii iliporipotiwa na vyombo vya habari,” alisema Bi JumaBw Sagana alisema mshtakiwa huyo hana mapato na kuomba korti izingatie kupitisha atumikie kifungo cha nje.

Bw Kimutai aliyemwakilisha  Bw Soi alisema alistaafu kutoka idara ya polisi  siku ile alitiwa nguvuni.Alisema hakufaidi na pesa hizo na kuomba mahakama itilie maanani umri wake wa miaka 65 na athari za ugonjwa wa Covid-19 kwa uchumi wa kila mtu.

“Mshtakiwa alistaafu 2016 na kwa sasa hana mapato. Naomba korti itilie maanani kazi aliyofanya akiwa afisa wa polisi na kiongozi wa timu iliyowakilisha Kenya Olimpiki,”alisema Bw Kimutai

Bi Juma aliwaagiza walipe faini hiyo akisema , “ sheria inampasa awaadhibu washtakiwa waliotakiwa kuwa waaminifu kutunza na kusimamia pesa za umma.”Aliwapa siku 14 kukata rufaa.

  • Tags

You can share this post!

‘Unywaji wa kahawa una madhara pia’

Malkia Strikers wang’aria Burundi mtihani mkali dhidi ya...