• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Wauguzi 66 watuzwa kwa kazi nzuri ya kuwashughulikia wagonjwa hospitalini Gertrude’s

Wauguzi 66 watuzwa kwa kazi nzuri ya kuwashughulikia wagonjwa hospitalini Gertrude’s

NA LAWRENCE ONGARO

WAUGUZI 66 wa kushughulikia watoto wametambuliwa kwa kazi nzuri ya kuwashughulikia watoto wagonjwa katika hospitali ya Gertrude’s Children’s Hospital jijini Nairobi.

Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Gertrude’s Dkt Robert Nyarango aliwapongeza na kuwahimiza kujituma kazini.

Wauguzi Dulo Naomi Akinyi na Khan Nasra Ismail ni miongoni mwa waliopokea tuzo maalum.

Wauguzi hao wapya ni miongoni mwa wengine 130 ambao walifuzu kutoka katika hospitali hiyo.

Wengi walipata ujuzi wa utafiti wa kimaabara na pia malezi ya kawaida.

Kulingana na mkurugenzi huyo, hatua hiyo ni mojawapo ya mwelekeo mzuri wa kupata wauguzi wenye ujuzi wa kuwashughulikia watoto wagonjwa.

Mkurugenzi huyo alisema wauguzi wapatao 240 huhitajika kushughulikia wagonjwa 100,000.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ya tuzo ni mkuu wa utafiti kuhusu maswala ya maradhi ya watoto Perez Obonyo na msimamizi wa maswala ya hospitali Prof Elizabeth Obimbo.

Wakuu wa hospitali hiyo walisema inatoa matibabu ya hali ya juu, wakisema ina madaktari na wauguzi stadi.

  • Tags

You can share this post!

Walioachiliwa kuhusiana na mauaji ya dereva wa teksi...

DONDOO: Bodaboda ashtua demu kufika kwake alfajiri na...

T L