• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Yaya afungwa miaka miwili kwa kuiba mikufu

Yaya afungwa miaka miwili kwa kuiba mikufu

Na RICHARD MUNGUTI

MJAKAZI aliyeiba mikufu ya dhahabu iliyo na thamani ya Sh300,000 na kufungwa miaka miwili jela hajakata rufaa.

Rebeca Isiche Elumbe aliyetorokea mji wa Eldoret kabla ya kukamatwa alirudishwa Nairobi kushtakiwa baada ya polisi kuchapisha yake katika vyombo vya habari.Mbali na mikufu hiyo mshtakiwa pia alimwibia mwajiri wake simu iliyo na thamani ya Sh40,000 na pesa tasilimu Sh90,000.

Isiche alishtakiwa pamoja na mpenzi wake Kennedy Kimanthi mbele ya hakimu mwandamizi Bw Peter Mutua.Mahakama ilifahamishwa na kiongozi wa mashtaka kuwa Isiche aliiba mali hiyo kutoka makazi ya mwajiri wake Maryann Abdi iliyo na thamani ya Sh430,000.

Hakimu alifahamishwa Isiche alifululiza moja kwa moja hadi kwa makazi ya mpenziwe alipokesha kisha akampa Sh1,000 akiondoka kwenda  Eldoret.Mshtakiwa alikuwa akiishi pamoja na mwajiri wake katika makazi ya Royal Park Apartments.

Alikuwa amefanya kazi miezi miwili kabla ya kuchomoka na pesa hizo na mikufu mnamo Agosti 2 2021.Isiche aliondoka katika makazi hayo ya mwajiri wake mwendo wa saa tano asubuhi.Bi Abdi alikuwa kazini mshtakiwa alipohepa na fedha hizo.

Alijituliza kwa Bw Kimanthi katika mtaa wa Umoja kwenye barabara ya Manyanja.Akiondoka alimwachia Bw Kimanthi Sh1,000 na simu hiyo ya kifahari.Kimanthi alieleza mahakama hakujua simu hiyo imeibwa na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh100,000 pesa tasilimu.

Alikana shtaka la kupatikana na mali aliyojua imeibwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.

 

  • Tags

You can share this post!

Baba na watoto washtakiwa kwa wizi wa Sh.54Milioni

Asukumwa jela miaka miwili kwa kupatikana na pingu