• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 3:23 PM
Zuma aapa kufichua waliomsaidia kumumunya mamilioni ya Afrika Kusini

Zuma aapa kufichua waliomsaidia kumumunya mamilioni ya Afrika Kusini

Na PETER DUBE

ALIYEKUWA rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameapa kuwa hatazama peke yake kwenye kesi za ufisadi zinazomkabili.

Zuma alisema ana habari za kina za kila mmoja wa maafisa wakuu wa chama cha ANC kuhusu ufisadi wa mamilioni ya pesa na uhalifu mwingine.

Aliambia tume inayochunguza mfumo wa ufisadi unaohusisha wanasiasa na wafanyibiashara nchini humo kuwa kumekuwepo na njama ya muda mrefu ya kumwangusha kisiasa,

Kiongozi huyo aliyejiuzulu urais kufuatia madai ya ufisadi, aliwataja maafisa kadhaa aliosema ni wafisadi na walishiriki katika njama ya kumhangaisha.

Alidai kuwa mfanyibiashara maarufu nchini humo, Johann Rupert alitishia kuzamisha nchi hiyo iwapo Zuma angemfuta kazi aliyekuwa waziri wa fedha, Pravin Gordhan.

Pia alidai kupewa vitisho na waziri wa uchukuzi, Fikile Mbalula.

Alisema pia kulikuwa na njama ya kumuua kwa kutumia wauaji waliokodishwa kutoka nje ya Afrika Kusini, lakini akanusurika alipokosa kwenda uwanjani mjini Durban, ambako alipangiwa kuuawa.

Hali ya wafisadi kuteka siasa na uchumi wa nchi pia imeshuhudiwa hapa Kenya ambapo mitandao inayoshirikisha wafanyibiashara wakubwa na wanasiasa imesababisha wizi wa mabilioni ya pesa za umma.

Mitandao hiyo imekuwa ikilipwa pesa zaidi ya zinazostahili kwenye miradi na pia kuzima wengine kupewa kandarasi.

You can share this post!

Aliyekuwa mtangazaji wa KTN akiri kuhadaa polisi

Ajuza asimulia korti jinsi mwanawe amekuwa akimcharaza

adminleo