Habari za Kitaifa

Takriban watu 10 wasombwa na maji wakijaribu kuvuka mto wakiwa ndani ya gari Makueni

April 26th, 2024 1 min read

NA PIUS MAUNDU

TAKRIBAN watu 10 wanashukiwa kuangamia baada ya kusombwa na mafuriko walipokuwa wanajaribu kuvuka Mto Muswii katika Kaunti ya Makueni.

Katika mojawapo ya video ambayo imenaswa na walioshuhudia, abiria waliokuwa kwenye gari lililozama wanaonekana wakijaribu kuogelea huku maji yaliyokuwa yanaenda kwa kasi yakiwalemea huku waliokuwa wanatazama wakipiga mayowe.

Hakukuonekana waliojaribu kuwaokoa kwa hofu ya kusombwa pia, wengi wao wakiwaambia kushikilia mti au chochote kinachoweza kushikilika.

Usafiri katika barabara ua Kasikeu-Sultan Hamud umekatizwa baada ya mto huo ambao unaanzia katika kaunti jirani ya Kajiado kuvunja kingo zake.

Jaribio la wakazi kuvuka kutumia lori lilisambaratishwa baada ya lori hilo kuanguka na kuzama majini.

Shughuli za uokoaji zinaendelea…