TALANTA YANGU: Kiongozi wa maskauti

TALANTA YANGU: Kiongozi wa maskauti

Na RICHARD MAOSI

KIONGOZI wa bendi ya maskauti anafaa kuwa na maono ya juu, wakati wa kutoa mwongozo ili kukipa kikosi chake mafanikio.

Isitoshe, maskauti wanahitaji bendi ya muziki ili kuongeza nakshi na uwiano katika gwaride ambalo mara nyingi hulenga kufurahisha umati.

Hii ndiyo kauli mbiu ya wanafunzi kutoka Gilgil Hills Academy inayopatikana katika eneo la Gilgil Kaunti ya Nakuru chini ya uongozi wa Joy Wairimu mwenye umri wa miaka 14.

Akiwa kiongozi na mwelekezi wa kikosi cha wanaskauti wa shule, anaungama kuwa amepata ujasiri mwingi.

Joy Wairimu mwenye umri wa miaka 14 kutoka Shule ya Msingi ya Gilgil Hills iliyoko Kaunti ya Nakuru ambaye ni kiongozi wa maskauti na bendi.
PICHA | RICHARD MAOSI

Wairimu anasema kuelekeza gwaride la maskauti pamoja na wanabendi si jambo rahisi. Kwanza kunahitaji ujuzi wa hali ya juu, bidii na nidhamu.

Aidha, anasema kuwa ushirikiano baina ya maskauti na wachezaji bendi ni jambo la kimsingi, la sivyo kikosi kinaweza kuvunjika.

Isitoshe, anasema bendi yake hutumiwa kuwatumbuiza wanafunzi wa shule ya Gilgil Hills kila siku ya Jumatatu na Ijumaa kwenye gwaride ama siku ya wazazi shuleni.

Anasema kuwa yeye huongoza kikosi cha washiriki 20 ambao ni wa kati ya umri wa miaka 8-14 ambao wengi wao wana maono ya kutumikia taifa katika daraja mbalimbali za uongozi siku za usoni, mojawapo ikiwa ni kitengo cha jeshi la wanahewa.

You can share this post!

Corona: Afrika Kusini sasa yadai ‘kuonewa’

PAUKWA: Biashara haramu ya Titi (sehemu 3)

T L