Tammy Abraham aweka rekodi mpya ya ufungaji wa mabao miongoni mwa wanasoka raia wa Uingereza katika Serie A

Tammy Abraham aweka rekodi mpya ya ufungaji wa mabao miongoni mwa wanasoka raia wa Uingereza katika Serie A

Na MASHIRIKA

TAMMY Abraham, 24, ameweka rekodi mpya ya mwanasoka raia wa Uingereza kuwahi kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) baada ya kupachika wavuni magoli mawili katika ushindi wa 3-0 uliosajiliwa na waajiri wake AS Roma dhidi ya Torino mnamo Mei 20, 2022.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea na Aston Villa alifunga bao lake la 16 na 17 katika Serie A msimu huu katika mchuano huo uliochezewa jijini Turin. Ilikuwa mechi ya mwisho kwa Roma kutandaza ligini msimu huu.

Rekodi ya awali ilikuwa ikishikiliwa na Gerry Hitchens aliyepachika wavuni mabao 16 akivalia jezi za Inter Milan mnamo 1961-62.

Roma walikamilisha kampeni zao ligini muhula huu katika nafasi ya sita kwa alama 63 na hivyo kufuzu kwa soka ya Europa League muhula ujao.

Abraham alijiunga na Roma mnamo Agosti 2021 baada ya kuagana na Chelsea kwa kima cha Sh5.3 bilioni.

Roma watacheza na Feyenoord katika fainali ya kipute kipya cha Europa Conference League mnamo Mei 25, 2022. Bao lao jingine dhidi ya Torino lilipachikwa wavuni na nahodha Lorenzo Pellegrini kupitia penalti ya dakika ya 78.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mkataba wa Ruto na Muturi wazimwa

Mbappe afunga mabao matatu dhidi ya Metz na kuibuka...

T L