TAMTHILIA: Maendelezo ya Onyesho la Tatu, Tendo la Kwanza – Kigogo

TAMTHILIA: Maendelezo ya Onyesho la Tatu, Tendo la Kwanza – Kigogo

JUMA lililopita tuliangalia onyesho la tatu, tendo la kwanza. Juma hili tutaendelea kulizamia kwa kina.

Muktadha wa onyesho hili ni ofisini kwa Mzee Majoka, wana mazungumzo ya faragha na mshauri wake Mzee Kenga. Majoka anachukua gazeti na kulifunguafungua kisha kugundua jambo fulani ambalo Kenga hakumjuza. Kuwa maoni ya wengi gazetini ni kwamba, Tunu apigiwe kura za kuongoza Sagamoyo. Kenga anashangaa (maudhui – ukosefu wa umakini).

Majoka anataka kujua wafadhili wa gazeti hilo. Kenga anamshauri Majoka kutangaza kuwa maandamano hayo ni haramu kisha polisi watumie nguvu na aache moyo wa huruma (maudhui – ukatili, mtindo – kinaya). Majoka anapinga wazo hilo. Kenga anamwambia Majoka kwamba maandamano hayo yangetia doa sherehe za uhuru na Tunu angezidi kupata umaarufu.

Kenga anasema yuko tayari kuwaweka waandamanaji pahali pao; mmoja baada ya mwingine, huenda wamesahau mauaji ya Jabali (sifa ya Kenga – muuaji).

Kenga anasema kuwa, ukitaka kuwafurusha ndege, kata mti. (mtindo – mdokezo wa methali).

Majoka anakubaliana na kauli ya Mzee Kenga. Kenga anadokeza kuwa, Tunu ana mpango wa kuleta wachunguzi kutoka nje kuangalia upya ajali ya Jabali. Majoka anashtuka (sifa ya Majoka – muuaji). Anasema uchunguzi huo uzuiliwe.

Kenga anakiri kuwa itawagharimu kwa sababu ya jumuiya. Itabidi watumie mbinu tofauti. Majoka anaamua kuwashughulikia Tunu na Sudi. Anajiita profesa wa siasa. Anasema hatatumia bomu kuua mbu (mtindo – msemo uk35).

Simon Ngige

Alliance High School

  • Tags

You can share this post!

Mtiririko wa vitushi na wahusika katika sura 10 –...

Tathmini ya hadithi ‘Mwalimu Mstaafu’

T L