TAMTHILIA: Mtiririko wa matukio katika Sehemu ya I, Onyesho la III

TAMTHILIA: Mtiririko wa matukio katika Sehemu ya I, Onyesho la III

JUMA hili tuangalie mtiririko wa matukio katika Sehemu I, Onyesho III.

Hapa ni nyumbani kwa Sara, jikoni. Mandhari huonyesha mahali. Dina anahangaika na jiko huku akiandaa mchuzi. Sara ameketi kwenye kiti kidogo akiwa amejikunyata.

Upishi huo unamfanya Sara kupata nafuu kwani kukosekana kwa chakula pale kunamfanya mumewe kumpa presha kutokana na maswali mengi ambayo Yona angemuuliza mkewe. Sara anamshukuru Dina kwa kuitikia wito alipomhitaji. (Uhusiano mwema).

Dina anamwambia Sara kuwa wanawake wanastahili kufaana. Dina na Sara wana maongezi ya kirafiki. Dina anamkumbusha Sara kuwa dunia ni uwanja wa mitihani na kumkumbusha umuhimu wa kuvumilia hasa watu wenye vinywa vichafu. Uvumilivu huo unazaa faraja.

Sara anamshukuru Mungu kwa wana aliomjalia na hasa kwa Neema ambaye amejitolea kumpeleka kwa matibabu yanayomrejeshea matumaini. Katika hospitali hiyo, kuna wataalamu hodari na madaktari waliomakinika sana. (Uwajibikaji kazini).

Sara anarejelea suala la kutukanwa kwa sababu ya kukosa kupata watoto wa kiume. (Utamaduni usiofaa). Alisimangwa hadharani na faraghani, makanisani, hata magengeni. Lakini kwa sasa akiwaona binti zake anaridhika sana moyoni kwa ufanisi wao maishani (Tumaini).

Hili linamfanya kutokwa na machozi. Maongezi haya ya kirafiki yanamfanya Dina kutotambua kuwa maji yalikuwa yamechemka kitambo. Dina anaanza kupika. Tunagundua kuwa Yona alitoka bila kumfahamisha mkewe alikokwenda.
Tunafahamu pia kuwa kabla ya kuja kwake na kuulizia chakula, alikuwa amepitia kwa mwenzake ambapo alipata pia hakukuwa na chakula huko…tutaendelea juma lijalo

Simon Ngige-Shule ya Upili ya Alliance

  • Tags

You can share this post!

Pwani: Kuna haja wazazi, serikali kulinda watoto dhidi ya...

Kunguni waongezeka katika lojing’i Kisumu

T L