TAMTHILIA: Uongozi mbaya katika Kigogo – 3

TAMTHILIA: Uongozi mbaya katika Kigogo – 3

JUMA hili tutaendelea kuangalia maudhui ya uongozi mbaya katika Tamthilia ya Kigogo.

Viongozi kupanga njama ili kuangamiza wapinzani wao; Majoka na Kenga wanapanga njama ya kumtia Ashua ndani.

Wanapanga aitwe ofisini mwa Majoka kisha Husda aitwe ili wazozane. Ashua anasingiziwa kuzua zogo katika ofisi ya serikali na kutiwa ndani. Husda anafunguliwa baada ya nusu saa.

Kifo cha Jabali kilipangwa. Jabali alikuwa mpinzani wa Majoka mwenye wafuasi wengi. Akapangiwa ajali barabarani kisha wafuasi wake wakazimwa na kumfuata jongomeo, chama chake cha Mwenge kilimfuata ahera.

Tunu anapanga kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali ya Jabali. Majoka anapopata habari hizi, anapanga kuzima uchunguzi huo.

Kenga na Majoka wanapanga kuondoa chatu mmoja. Wanahofia kutolewa uongozini na ili kuzuia hali hii, wanapanga kumwondoa mmoja wao.

‘…chatu mmoja atolewe kafara ili watu wajue usalama upo, wakereketwa waachwe katika hali ya taharuki.’

Majoka anapanga njama Tunu auawe, anaumizwa mfupa wa muundi. Nia yake ikiwa ni kumkomesha asimpinge.

Majoka anatumia polisi wake kutekeleza ukatili huo.

Katika hotuba ya Tunu anayowahutubia waandamanaji, Sagamoyo kuna uongozi mbaya.

Anasema kuwa; pesa za kusafisha soko zimefujwa, soko linafungwa badala ya kusafishwa, haki za wauzaji zimekiukwa. Viongozi hawasikilizi matakwa ya wananchi. Majoka hana wakati wa kuwasikiliza waandamanaji. Hataki kujua chanzo cha maandamano wala suluhu lake.

Simon Ngige

Alliance High School

You can share this post!

Kipa Kasper Schmeichel ajiunga na Nice baada ya kuondoka...

Magoha aomba radhi kwa kuagiza shule kufungwa ghafla

T L