Habari Mseto

Tanzia babake Jowie Irungu akiaga dunia mwanawe akihukumu kifungo cha maisha


BABAKE Joseph ‘Jowie’, Irungu,  Joseph Mwangi Irungu, amefariki dunia baada ya kuugua saratani kwa miaka mingi.

Mjane, Annastacia Thaama, amethibitisha kuwa mumewe alikata roho Jumamosi, Juni 15, 2024, katika Hospitali ya Nakuru Level Five Annex, mjini Nakuru alikolazwa baada ya ugonjwa huo kumlemea.

Mzee Irungu, 64, amewaacha mjane huyo mmoja na watoto wanne.

Mnamo Februari 9, mwaka huu Jowie alihukumiwa konyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mfanyabiasha Monica Kimani mnamo usiku wa kuamkia Septemba 18,2018.

Hata hivyo, mpenzi wake wa zamani, aliyekuwa mtangazaji wa habari kwenye runing Jacque Maribe, aliondolewa lawama.

Jaji wa Mahakama Kuu Grace Nzioka aliukosoa upande wa mashtaka kuwa kumshtaki Maribe “kwa kosa ambalo hakutenda.”

Mauaji ya Monica yaliibua kero kubwa nchini kwa sababu yalitekelezwa kinyama.

Alikatwa masikio, akafungwa mikono na miguu kabla ya koo yake kukatwa kwa kisu.

Jowie amekuwa akizuiliwa katika gereza la Industrial Area, Nairobi akisubiri kunyongwa.