Habari

TANZIA: Mshairi Abdallah Mwasimba afariki

July 29th, 2020 1 min read

Na HASSAN WEKESA

MZEE Abdallah Mwasimba ambaye ametunga na kughani mashairi kwa miaka mingi amefariki baada ya kuugua kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.

Sauti yake ilisikika katika vituo vya redio kama kile cha Shirika la Habari la Kenya (KBC) na vilevile mashairi yake yamechapishwa katika safu ya ushairi ya gazeti la Taifa Leo.

Amekuwa ni mwanaharakati wa lugha ya Kiswahili.

Mwanawe wa kiume, Mwasimba Abdallah, amethibitisha kwamba mzee ametangulia mbele ya haki wakati akiwa na umri wa miaka 83.

Alizaliwa mwaka 1937 eneo la Matuga, Kwale.

“Babangu ameaga dunia saa kumi kuamkia leo Jumatano,” amesema Mwasimba Jr.

Maziko ni leo Jumatano katika makaburi ya Kariakor kabla adhuhuri.