Makala

Tanzia: Mwanzilishi wa NIBS, Lizzie Wanyoike, aaga dunia

January 14th, 2024 1 min read

NA WANDERI KAMAU

MWANZILISHI wa Taasisi ya Mafunzo ya Kiufundi ya Nairobi Institute of Business Studies (NIBS), Bi Lizzie Wanyoike, ameaga dunia.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na familia yake saa chache zilizopita, Bi Wanyoike alifariki mnamo Jumapili, Januari 14, 2024.

“Kwa kumbukumbu ya mwanaelimu shupavu. Kujitolea kwake kuliwafaa wengi, ukarimu wake uligusa roho nyingi. Alikuwa nguzo ya uungwana. Ameacha mabadiliko makubwa katika maisha ya mamilioni ya watu, kwa kuboresha maisha yao ya baadaye kwa neema,” ikasema taarifa kutoka kwa familia hiyo.

Juhudi za Taifa Leo Dijitali kujaribu kuwasiliana na familia yake, wasimamizi wakuu wa taasisi hiyo na washirika wake wa karibu hazikufua dafu.

Bi Wanyoike alizaliwa mnamo Novemba 28, 1951.

Hata hivyo, duru zilitueleza kuwa marehemu amekuwa akiugua Saratani.