Habari

Tathmini ya KNBS yaonyesha viwango vya juu vya umaskini Kenya

August 11th, 2020 1 min read

Na CHARLES WASONGA

ZAIDI ya nusu ya Wakenya wanaishi katika lindi la umaskini, kulingana na matokeo ya tathmini ya kipekee iliyofanywa na Shirika la Kitaifa kuhusu Takwimu (KNBS).

Utafiti huo ambao ulichunguza vigezo vingine kando na ukosefu wa pesa, imebaini kuwa asilimia 53 ya Wakenya ni masikini, tafauti na asilimia 36.1 ikiwa kigezo cha fedha pekee ndicho kitatumiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa KNBS Zacharia Mwangi alisema Jumatatu kwamba kando na fedha, utathmini huo ulimulika vigezo vingine kama vile, upatikanaji wa maji safi, elimu, umeme, chakula miongoni mwa vigezo vingine sita.

“Mtu atasawiriwa kuwa masikini ikiwa atakosa mahitaji matatu au zaidi ya kuweza kuimarisha maisha ya mwanadamu,” akasema.

Ripoti hiyo kwa jina ‘Comprehensive Poverty Report’ ilitayarishwa

Waziri wa Fedha Ukur Yatani ambaye alizundua ripoti hiyo Jumatatu alisema kuwa changamoto inayowakabili watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ni pamoja na ukosefu wa makazi salama, lishe bora na mazingira safi na salama kwa ujumla.

Na miongoni mwa watu wazima, ukosefu wa elimu, nyumba na kazi zenye mapato ndivyo huchangia pakubwa umaskini miongoni mwa wanawake na wanaume nchini Kenya.