Team Control yabanwa Maluda Super Cup

Team Control yabanwa Maluda Super Cup

Na CHARLES ONGADI

MAJAONI Youngsters FC iliilazimisha Team Control sare tasa katika mchuano wa kuvutia wa Maluda Super Cup uwanjani Harare, Shanzu, mjini Kisauni.

Licha ya kuchezesha wachezaji wengi wenye majina makubwa, Team Control ilishindwa kukabiliana na wepesi wa chipukizi wa Majaoni Youngsters katika mechi hiyo ya Jumatatu. Akizungumza baada ya pambano hili, kocha wa Majaoni Youngsters Khama Kamau alisema kwamba aliwashauri wachezaji wake kucheza mchezo wa kasi ili kuwalemea wapinzani wao walio na umri mpevu.

‘Siri yangu ilikuwa kuwachezesha wachezaji chipukizi na wenye kasi dhidi ya wapinzani wetu ambao wengi wao wanajivunia ujuzi wa siku nyingi ila hawana kasi kutokana na umri kuwazong,’ akasema kocha Kamau. Hata hivyo, kulingana na mwenzake kocha Gerishon Kanga ni kwamba sare hiyo ilitokana na baadhi ya wachezaji wake tegemeo kukosekana kikosini kutokana na majeraha.

Kati ya wachezaji mahiri waliochezea Team Control ni aliyekuwa golikipa wa timu ya taiifa na Bandari FC Wilson Oburu na difenda Evans Orodi ambaye pia aliyewahi kuichezea timu ya taifa, Harambee Stars.Katika pambano lengine la kuwania taji hili iliyogaragazwa ugani Hassa Joho Girls, Utange, Shimo Annex FC iliikomoa Olympiakos 4-1.

Annex inayonolewa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya vijana (U17) Nathaniel Malau, ilipata mabao yake mapema kupitia ian kombo Nassoro Ali aliyepachika mawili na Fikirini Katana.

Katika mchuano wa ligi ya FKF Mombasa kwenye uga wa Bilima, Pasi Moja FC ilikung’uta Rising Stars 4-1.Magoli yake yalifungwa na Henry Mwangemi, Willy Maube, Nickson Okila na Edward Kenga huku John Kakonge akifungia Rising Stars la kufutia machozi.

You can share this post!

Sharks, Homeboyz zalenga kupanua uongozi ligini leo

Koth Biro mechi mbili kuchezwa Alhamisi

T L