Team Kenya ya Davis Cup tayari kwa Kombe la Afrika tenisi

Team Kenya ya Davis Cup tayari kwa Kombe la Afrika tenisi

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya tenisi ya wanaume ya Kenya imekamilisha matayarisho na kupokea bendera ya taifa tayari kuondoka nchini kushiriki Kombe la Afrika la Davis Cup kundi la III nchini Algeria mnamo Agosti 10-13.

Wachezaji watakaowakilisha Kenya ni Albert Njogu, Derick Ominde, Keean Shah na Kael Shah. Wazoefu Ibrahim Kibet, Kevin Cheruiyot na Ismael Changawa wametupwa nje.Watatu hao walikuwa wamewakilisha Kenya kwa muda mrefu.

Shughuli ya kupewa bendera ilifanywa na nabu rais wa Shirikisho la Tenisi Kenya Philip Ilako, ambaye aliwahi kuwakilisha Kenya kwenye Davis Cup enzi zake, na mweka hazina Rose Wanjala, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya voliboli kwenye michezo ya Afrika 1987 jijini Nairobi.

Kocha Francis Rogoi ndiye nahodha wa timu ya Kenya itakayokabiliana na Algeria, Benin, Ivory Coast, Morocco, Msumbiji, Namibia na Zimbabwe.

Mataifa tatu-bora yatajikatia tiketi kushiriki mashindano ya kuingia Kundi la Tatu la Dunia. Timu mbili za mwisho zitashushwa ngazi hadi Kombe la Afrika Kundi la Nne. Timu itasafiri Agosti 6.

  • Tags

You can share this post!

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Maulana atujaalie tuwe na uchaguzi wa...

Okutoyi asalimu amri robo-fainali ya wachezaji wawili...

T L