Teknolojia yameza 60% ya mapato ya maajenti wa utalii

Teknolojia yameza 60% ya mapato ya maajenti wa utalii

Na BERNARDINE MUTANU 

Maajenti wa kimapokeo katika sekta ya utalii wanazidi kuumia kutokana na ujio wa teknolojia. 

Wanapoteza hadi asilimia 60 ya soko kutokana na kuwa watalii sasa wanajihifadhia nafasi katika maeneo wanayotaka kutalii kwa kutumia mitandao na simu. 

Kulingana na Chama cha Maajenti wa Usafiri (KATA) wamepoteza asilimia kubwa ya soko katika muda wa miaka 10 iliyopita. 

Hiyo ni kumaanisha wanapoteza Sh39 milioni kila mwakakilisema chama hicho. Kwa sasawatumiaji wa intaneti nchini ni milioni 36.09 kulingana na Tume ya Mawasiliano. 

HivyoWakenya wengi wanapata habari kuhusiana na sekta hiyo kwa mtandaona hawahitaji tena mawakala kuwahifadhia mahoteli au hata ndege. 

Mawakala hao sasa wameachiwa watu wanaosafiri kufanya biashara.

You can share this post!

Pasta alitunga mimba mwanafunzi wa darasa la 7, DNA...

Wanaofanya biashara na mashirika yasiyo na PIN ya KRA...

adminleo