Tetesi: Arsenal, Dortmund wamezea mate beki Okumu

Tetesi: Arsenal, Dortmund wamezea mate beki Okumu

Na GEOFFREY ANENE

BEKI wa KAA Gent nchini Ubelgiji, Joseph Stanley Okumu amesherehekea kufikisha umri wa miaka 25 mnamo Mei 26 akihusishwa na uhamisho na klabu ya Arsenal (Uingereza), Celtic (Scotland) na Borussia Dortmund (Ujerumani).

Kwa mujibu wa gazeti la People Daily, hata hivyo, mabingwa wa zamani wa Ujerumani Dortmund ndio wameonyesha hamu zaidi kwa kuulizia rasmi huduma za nyota huyo mrefu maarufu kama Crouch.

“Okumu yuko wazi kuhamia Dortmund muradi makubaliano yanayofaa yaafikiwe,” gazeti hilo likinukuu mmoja wa mawakala wake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chemelil Sugar (Kenya), Free State Stars (Afrika Kusini), Ann Arbor na Real Monarchs (Amerika) alijiunga na KAA Gent mnamo Julai 1 mwaka 2021 kwa Sh437.7 milioni kutoka Elfsborg nchini Uswidi. Amechezea Gent jumla ya michuano 47 msimu 2021-2022 ikiwemo 27 kwenye Ligi Kuu (Jupiler Pro League) na kuchangia mabao manne.

Katika kipindi amekuwa Gent, thamani yake imepanda hadi Sh562.7 milioni kwa hivyo klabu yoyote itakayofaulu kumnyakua italazimika kumwaga mamilioni zaidi ya shilingi kupata huduma za Okumu aliyewahi kulinganishwa kimchezao na Mholanzi Virgil van Dijk anayesakatia Liverpool, Uingereza. Gazeti hilo linasema kuwa Okumu anatarajiwa nchini Kenya mnamo Mei 26 kuhudhuria mazishi ya nyanyake katika kaunti ya Busia.

  • Tags

You can share this post!

Liverpool wamsajili kinda matata wa Fabio Carvalho kutoka...

Mourinho aongoza AS Roma kutandika Feyenoord na kutwaa taji...

T L