Habari Mseto

Thamani ya shilingi ya Kenya yaporomoka

November 19th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Shilingi ya Kenya imeendelea kupoteza thamani yake dhidi ya dola ya Marekani.

Kufikia Alhamisi, dola moja ilikuwa ni Sh103 za Kenya, thamani ya chini zaidi tangu Januari.

Kulingana na soko la humu nchini, thamani ya shilingi dhidi ya dola ilikuwa ni Sh103.25. Kulingana na wachanganuzi wa masuala ya kifedha, hali hiyo ilisababishwa na mahitaji ya juu ya dola hasa kutoka kwa waagizaji wa mafuta.

Mara ya mwisho kwa thamani ya shilingi kuwa dhaifu kiwango hicho dhidi ya dola ilikuwa ni Januari 17, 2018.