Habari

Theresa May atangaza atajiuzulu Juni 7

May 24th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Theresa May, ametangaza Ijumaa kwamba atajiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative ifikapo Juni 7, akikiri pia kwamba alishindwa kupata mkakati mzuri wan chi yake kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

“Litabaki suala la mimi kulisikitikia kwamba sijafanikiwa kufanikisha mchakato wa Brexit,” May amesema nje ya Downing Street.

Tayari amemfahamisha Malkia Elizabeth II kuhusu uamuzi huo.

“Mimi ni Waziri Mkuu wa kike wa pili; na bila shaka sio wa mwisho,” amesema May akibubujikwa na machozi.

Kiongozi mpya wa Conservative atarithi wadhifa wa Waziri Mkuu.