TIBA NA TABIBU: Mitandao ya kijamii yaanza kuteka watoto wa shule za msingi na kuwanyima usingizi

TIBA NA TABIBU: Mitandao ya kijamii yaanza kuteka watoto wa shule za msingi na kuwanyima usingizi

NA WANGU KANURI

WANAFUNZI wa shule za msingi wanapoteza usingizi wa usiku mmoja kila wiki sababu ya kukaa macho wakipekua mitandao ya kijamii.

Hii ni licha ya wanafunzi hao wenye miaka 10 kupendekezwa kupata saa tisa hadi kumi za usingizi kila usiku huku kutopata usingizi wa kutosha kukihusishwa na matokeo mabaya darasani.

Utafiti uliowachunguza wanafunzi 60 ulionyesha kuwa asilimia 89 wengi wao walitumia simu zao kupekua mitandao ya kijamii ya TikTok, Instagram, Reddit na Facebook.

Ili kupata matokeo ya utafiti wao, wanasayansi hao waliwauliza wanafunzi hao ni wakati gani wao huenda kulala, walilala na kuamka saa ngapi na ni mara ngapi walizima saa ya kengele ilipolia.

“Utafiti ulionyesha kuwa ubora wa usingizi wao ulidorora kulingana na muda waliotumia wakipekua mitandao ya kijamii.”

Wanafunzi hao walieleza kuwa walihisi kama wamejitengana na marafiki wao kama hawapo kwenye mitandao ya kijamii.

“Wengi wao walipata wasiwasi wa kutokuwa kwenye mtandao huku wakihusisha wasiwasi huo na kutojua au kutoshiriki na mambo yaliyokuwa yakiendelea humo,” watafiti wanaeleza.

Hata hivyo, wanasayansi wanawashauri wazazi kupima wakati ambao watoto wao haswa wanafunzi wanatumia wakipekua mitandao ya kijamii kwa chini ya saa mbili kwa siku.

  • Tags

You can share this post!

JIJUE DADA: Uchungu kwenye matiti ni tatizo la wengi

Napiga chafya kupindukia, mbona?

T L