TIBA NA TABIBU: Wanasayansi watahadharisha kuhusu uraibu wa simu

TIBA NA TABIBU: Wanasayansi watahadharisha kuhusu uraibu wa simu

NA WANGU KANURI

IWAPO unatumia simu yako kupekua mtandao, kucheza michezo mbalimbali, kupiga gumzo, kuangalia baruapepe kwa muda mrefu kwa siku badala ya kuzungumza na watu walio karibu nawe, basi wewe umekuwa mraibu wa simu.

Zaidi na matumizi haya ya simu kuathiri utendakazi wa mtu, mahusiano hudorora huku wanasayansi kutoka Uingereza wakiwapa waraibu hawa namna ya kupunguza muda wanaotumia kwa simu.

Utafiti wao ulionyesha kuwa kutumia muda mchache kwa simu hata kwa saa moja kwa siku, humsaidia mtu kutokuwa na wasiwasi na kumpa muda wa kufanya mazoezi.

Hata hivyo, ili kupambana na uraibu huo, wanasayansi wanashauri kuwa mtu anapaswa kuficha apu anazotumia kwa muda mwingi na kuzirejesha pindi tu anapotaka kuzitumia.

Pia, mtu anapaswa kutengeneza ratiba ya shughuli au kazi anazopaswa kufanya kila siku na awe na nidhamu ya kuifuata.

Isitoshe, anapaswa kuwa na sheria nyumbani za nyakati za kutumia simu.

“Kwa mfano kutoruhusu wanafamilia wake kuwa na simu wakati wa maankuli au kwa saa kadhaa kwa siku kutasaidia kupunguza uraibu huu wa simu,” wanaeleza.

  • Tags

You can share this post!

Bodi kuchunguza wanaouza dawa bila ushauri wa daktari

DKT FLO: Homa ya mapafu inavyosambaa mwilini, dalili na...

T L