TIBA NA TABIBU: Wasiwasi huku idadi ndogo ikijitokeza kupimwa kansa ya mlango wa uzazi

TIBA NA TABIBU: Wasiwasi huku idadi ndogo ikijitokeza kupimwa kansa ya mlango wa uzazi

NA LEONARD ONYANGO

WATAALAMU wameelezea wasiwasi wao kuhusu idadi ndogo ya wanawake wanaofanyiwa vipimo vya kansa ya mlango wa uzazi (cervical cancer) humu nchini.

Dkt Anisa Mburu, mtaalamu wa maradhi ya saratani katika Hospitali ya Aga Khan, Mombasa na Kituo cha Kansa cha Kimataifa (ICI), anasema kuwa ni asilimia 15 tu ya wanawake wanaopimwa kansa ya mlango wa uzazi badala ya asilimia 70 inayopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Anasema kuwa wanawake zaidi ya 30,000 hupatikana na kansa ya mlango wa uzazi humu nchini kila mwaka.

“Kenya hupoteza wanawake 5,000 kutokana na kansa ya mlango wa uzazi kila mwaka. Inasikitisha kuwa ni asilimia 15 ya wanawake wanapimwa. Ugonjwa huo ukigunduliwa mapema unaweza kutibiwa na kupona,” anasema Dkt Anisa.

Virusi vya papillomavirus (HPV) ni kati ya visababishi vikuu vya kansa ya mlango wa uzazi.

Wataalamu wanaamini kuwa chanjo ambayo imekuwa ikitolewa nchini dhidi ya HPV miongoni mwa wanawake, haswa wasichana ni njia mojawapo ya kupunguza visa vya kansa ya mlango wa uzazi nchini.

Shirika la WHO wiki iliyopita lilisema kuwa dozi moja ya chanjo ya HPV inatosha.

Hiyo inamaanisha kuwa watu wanaopewa dozi moja ya chanjo hiyo hawahitaji dozi ya pili.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Upangaji uzazi umeongezeka, lakini elimu...

JIJUE DADA: ‘Coil’ isipokaa vizuri utahisi uchungu...

T L