Timbe atwaa Kombe la FA Thailand

Timbe atwaa Kombe la FA Thailand

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Ayub Timbe Masika alitwaa taji lake la pili nchini Thailand baada ya timu yake ya Buriram United kupiga Nakhon Ratchasima 1-0 katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Thammasat mjini Khlong Luang, Jumapili.

Masika alichezeshwa dakika 68 kabla ya nafasi yake kutwaliwa na Suphanat Muenta katika mechi hiyo ambayo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia Jonathan Bolingi alipachika bao la ushindi dakika ya 115.

Winga huyo alijiunga na Buriram mnamo Desemba 3, 2021 kwa kandarasi itakayokatika Mei 31, 2023.

Alishinda taji la kwanza mnamo Mei 4 baada ya waajiri hao wake wapya kukamilisha Ligi Kuu ya msimu 2021-2022 kwa alama 62, pointi mbili mbele ya washindi wa 2020-2021 Pathum United.

Masika ana uraia wa Ubelgiji baada ya kuishi nchini humo tangu 2006. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amecheza soka katika kiwango cha juu nchini Ubelgiji, Uchina na Japan, lakini mafanikio makubwa amepata katika kipindi kichache amekuwa Thailand.

  • Tags

You can share this post!

Muthama akwepa tena kampeni za Ruto Machakos kwa sababu ya...

Mkataba wa Ruto na Muturi wazimwa

T L