Michezo

Timu 50 za kimataifa kushiriki mashindano ya voliboli Eldoret

May 22nd, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

ZAIDI ya timu 50 kutoka mataifa sita zimetoa ithibati ya kuwania ubingwa wa mashindano ya kimataifa ya voliboli ya Amaco mwaka 2018 mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu.

Katika hafla ya kuzindua makala haya ya 12 jijini Nairobi hapo Mei 21, 2018, wadhamini kampuni ya bima Amaco wamesema timu kutoka Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Burundi na Sudan Kusini zitashiriki.

Amaco imetangaza kufadhili makala haya kwa jumla ya Sh9.3 milioni, huku tuzo ya washindi ikiongezwa kutoka 450, 000 mwaka 2017 hadi Sh600, 000 mwaka 2018.

Wenyeji Kenya walishinda makala ya 11 kupitia Kenya Prisons (wanawake) na General Service Unit (wanaume).

Mashindano haya yalianzishwa mwaka 2005 na Mkenya Paul Bitok, ambaye ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda tangu mwaka 2008.