Timu ya Kenya ya Olimpiki yapokea chanjo ya pili ya Covid-19

Timu ya Kenya ya Olimpiki yapokea chanjo ya pili ya Covid-19

Na GEOFFREY ANENE

WANAMICHEZO watakaowakilisha Kenya kwenye Olimpiki nchini Japan mnamo Julai 23 hadi Agosti 8 wamepokea chanjo yao ya pili ya Covid-19.

Wachezaji hao kutoka fani za taekwondo, raga ya wachezaji saba kila upande, ndondi na voliboli ya wanawake, walipokea chanjo hiyo Jumanne katika uga wa kimataifa wa Kasarani mjini Nairobi.

Waziri wa Michezo Amina Mohamed alikuwepo wakati wa zoezi hilo ambapo pia alipata kuzungumza na wachezaji na makocha wao kuhusu maandalizi yao ya michezo hiyo ya haiba itakayofanyika mjini Tokyo.”Tumepeana chanjo ya pili ilu kulinda wanamichezo wetu dhidi ya ugonjwa wa Covid-19,” Wizara ya Michezo ilisema Jumatano.

Kenya ilifaa kutoa chanjo ya pili mwezi Mei, lakini serikali ikaongeza kipindi cha kupeana dozi hiyo hadi wiki 12 baada ya India kupiga marufuku kusafirishwa kwa chanjo hiyo kufuatia ongezeko kubwa la virusi vya corona nchini.Chanjo ya kwanza ilitolewa kati ya Aprili 7 na Aprili 14.

Wakenya 90 wamefuzu kushiriki michezo ya Olimpiki wakiwemo pia waogeleaji Danilo Rosafio na Emily Muteti wanaofanyia mazoezi yao nchini Uingereza na Amerika wanakosoma katika Chuo Kikuu.

Timu ya marathon ilichaguliwa Februari ikiwa na washikilizi wa rekodi za dunia Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei, miongoni mwa wengine. Ile ya riadha za uwanjani itajulikana Juni 17-19.

  • Tags

You can share this post!

Wolves wamteua kocha Bruno Lage kujaza pengo la mkufunzi...

Ondoa chunusi usoni kwa kutumia maji ya mshubiri(Aloe vera).