Michezo

Timu za NSL zategemea vifaa moto msimu huu

September 17th, 2019 3 min read

Na JOHN KIMWERE

KINYANGÁNYIRO cha kuwania taji la Supa Ligi ya Taifa (NSL) kinapigiwa upatu kuzua msisimko wa kufa mtu baada ya timu shiriki kufanya usajili wa vifaa balaa tayari kwa kazi ya msimu huu wa 2019/2020.

Timu zote zimepania kuteremsha makabiliano makali kufukuzia tiketi ya kufuzu kupandishwa ngazi kushiriki Ligi Kuu ya KPL muhula ujao.

Ushuru FC inayosaka tiketi hiyo kwa hamu na ngamu baada ya kuteremshwa miaka minne iliyopita inajivunia kunasa huduma za wanasoka nane wapya kando kuweka katika kaburi la sahau kocha mpya, James James ‘Odijo’ Omondi.

Hata hivyo Mt Kenya United iliyoshushwa msimu uliyopita imeweka rekodi kwa kusajili idadi ya wachezaji 24 ikifuatia na Shabana iliyonasa wanasoka 20. Shabana FC na Migori Youth zinaongoza kwa kusajili wachezaji wanne na watatu wa kigeni mtawalia.

Shabana imetwaa Gnaba Vnane, Emmanuel Nwanko, Traore Abou na Coulibaly Mohamed (wote hawana klabu) kutoka Congo. Nayo Migori imewaleta Ally Ramadhan(Isanga Rangers, Tanzania), Ronald Mendo (Five Stars, Uganda) na Paul Liambo (Migori Youth Talent Academy, Ivory Coast). Bila shaka mpango mzima utaeleweka tu maana huu ndiyo usajili wa timu zote 10 ambazo zimekamata kumi bora baada ya kucheza mechi tatu.

NAIROBI STIMA

Imenasa huduma za Dennis Alusiola (Posta Rangers), Moses Ouma (Mt Kenya United FC), Christopher Bukach (Kibera Black Stars), Adam Said (St Josephs Youth FC), Francis Oduor (Shabana FC), Nicholas Omondi (Chemelil Sugar FC), Ibrahim Ahmed (Thika United FC), Caleb Olilo (Buruburu Sports FC), Fredrick Maina (hana klabu), Fredrick Ojwang (Ushuru FC), Alvin Mangeni (Kenya Police FC).

NAIROBI CITY STARS

Wesley Onguso (Posta Rangers), Wycliffe Otieno (Kariobangi Sharks FC), Anthony Kimani (Bandari FC), Levis Opiyo (Vihiga United FC), Nahashon Thiong’o (Mt Kenya United), Cornelius Mwangi, Stephen Mweni wote(Modern Coast Rangers), Elvis Noor (Kibera Black Stars), Eric Ochieng (Wazito FC), Salim Abdallah (AFC Leopards), Vincent Otieno (Hakati Sportiff), Jimmy Bageya (hana klabu, Uganda).

USHURU FC

Douglas Wamalwa, Bonface Makhacha, Joseph Maina wote (hawana klabu), Sebastian Osodo (FC Talanta), Nashon Nanyendo (Tusker FC), Dennis Waweru (Eldoret Youth), David Mwangi (Sony Sugar), Charles Okeyo (Bidco United).

FC TALANTA

Anthony Oginga (Nairobi Stima), Phelix Ouma, Michael Jairo, Erick Otieno wote (Kariobangi Sharks U-23), Patrick Andrea, Dennis Chimamo wote (Acakoro Football Academy), Telvin Maina (Kangemi Allstars), Bramwel Kavaya (Jericho Allstars).

VIHIGA UNITED

Hillary Otieno, Kevin Omondi wote (AP), Michael Odongo, Kelvin Odongo wote (Thika United), Mark Okola (Kenyatta University), Richard Iguza (Vihiga Sportiff FC), Lesley Owino (Kariobangi Sharks U-23), Morgan Ambuka, Junior Adeyefa wote (Chemelil Sugar FC), Alex Waiswa (Kisumu Allstars), Abisalom Onyango (Migori Youth FC), Samuel Tawayi (Ebwali High School), Kevin Djako (Academic Guipe Viviane, Ivory Coast).

BIDCO UNITED FC

Imetwaa Eric Gichimu (Mwiki United), Anthony Simasi (Eldoret Youth FC), Stephen Obukui (Mt Kenya United FC), Peter Ndungú (GDC FC), Kassim Mwinyi (Wazito FC), David Orem (Wazito FC), Emmanuel Mogaka (FC Talanta), Castro Ogendo(Gor Mahia FC), Eliud Emase (Posta Rangers), Henry Omollo (Thika United).

FORTUNE SACCO FC

Vincent Owino (Karatina Homeboyz), Brian Omondi na Quelen Awange wote (hawana klabu), Ziyadi Kiwanuku (hana klabu, Uganda), Dismas Odhiambo (Jericho Allstars), Jacob Wangui (Mukinduri FC), Malvin Nderitu (Dandora Asentos), Dennis Munyingi (Kabonge FC), Evans Mukhuba (Nairobi City Stars), Tedian Atuto (Bidco United FC), Kenneth Otieno (FC Talanta), Reuben Mangi (Murang’a Seal FC).

KIBERA BLACK STARS

Philip Okayo (Mt Kenya United FC), Amadiwa Neville, Kahn Blessing na Gilbert Alango wote (hawana klabu), Godfrey Murugi na Hillary Odhiambo wote (Gogo Boys FC), William Oricho (Wazito FC), Bill Okumu (Vapor Sports), Robinson Amule na Maclaurde Odali wote (Kenya Police FC).

MT KENYA UNITED FC

Ferdinand Nyongesa, Samson Ndegwa wote(Wazito FC) , Kevin Ndiwa (Hakati FC), Samwel Kabuthi, Omar Adisa wote (KCB FC), Benson Wasike (Wajiji FC), Dominic Oyando (Tandaza FC), Mohammed Njuguna (Mwiki United), Morgan Oduor, Francis Imbaya wote (Posta Rangers FC), Simon Namaswa, Alex Kakindu, Kevin Ndung’u wote (Jericho Allstars), Innocent Abwori (Nairobi City Stars), Eric Kipkirui (St Josephs Youth), Bernard Omollo (Tusker Youth), Kevin Oreso (Buruburu Sports), Edwin Wanjala (Chemelil Sugar FC), Peter Okoth, Boniface Kimani, Gregory Nyapala wote (Kangemi Allstars), Emmanuel Onyancha (Bidco United), Clement Masakidi (Kakamega Homeboyz, Congo), Hussein Seif (Fortune Sacco.