Tineja adaiwa kumuua na kumkata kichwa nyanya yake

Tineja adaiwa kumuua na kumkata kichwa nyanya yake

Na SAMMY WAWERU

MWANAMUME mmoja eneo la Kilo, Nyalenda Kaunti ya Kisumu aliwashangaza wakazi Jumatatu kwa kumuua nyanya yake kwa kumkata kichwa katika hali isiyoeleweka.

Mshukiwa huyo na ambaye anakisiwa kuwa na umri wa miaka 19 anasemekana baada ya kumuua nyanya yake, alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Kisumu ya Kati akiwa amebeba kichwa cha mwendazake.

Duru zinaarifu kwamba alikitia kwenye mfuko wa kubebea bidhaa.

Aliwashangaza maafisa wa polisi alipoarifu mmoja wao kutazama kilichokuwa kwenye mfuko aliokuwa nao.

Walipigwa na butwaa kugundua ulikuwa na “kichwa cha binadamu”.

Aidha, mshukiwa huyo alirejeshwa eneo la mkasa, Kilo ambapo maafisa wa polisi walichukua sehemu ya mwili iliyosalia.

Kiini cha kutekeleza kitendo hicho cha unyama hakijabainika, huku uchunguzi ukianzishwa na mshukiwa kutiwa mbaroni.

You can share this post!

Mpenziwe Tecra alimtishia mlinzi, mahakama yaambiwa

ODM yaenda kortini kupinga matokeo ya kura za Matungu