Michezo

Tineja Ansu Fati aweka historia ya ufungaji wa mabao Barcelona

October 3rd, 2020 2 min read

Na CHRIS ADUNGO

CHIPUKIZI Ansu Fati aliweka historia ya kuwa mwanasoka wa pili mwenye umri wa miaka 17 kufungia Barcelona jumla ya mabao 10 kwenye Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Hii ni baada ya nyota huyo mzawa wa Guinea-Bissau na raia wa Uhispania kufunga bao moja na kusaidia waajiri wake Barcelona kuwapepeta Celta Vigo 3-0 ligini mnamo Oktoba 1, 2020.

Fati alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 11 baada ya kupokezwa krosi safi na kiungo Philippe Coutinho. Goli hilo la Fati lilikuwa lake la tatu kutokana na mechi mbili za ufunguzi wa msimu huu wa 2020-21 katika La Liga.

Chini ya kocha Ronald Koeman, Barcelona walijipata wakisalia na wachezaji 10 pekee uwanjani kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza baada ya beki Clement Lenglet kuonyeshwa kadi nyekundu kwa makosa mawili ya kadi za manjano.

Presha kutoka kwa Barcelona mwanzoni mwa kipindi cha pili kulishuhudia Lucas Olaza akijifunga baada ya kutia kimiani krosi ya nahodha wa Barcelona, Lionel Messi katika dakika ya 51.

Sergi Roberto aliwafungia Barcelona bao la tatu lililozamisha kabisa chombo cha wenyeji wao mwishoni mwa kipindi cha pili.

Celta nusura wafunge bao wakati mambo yakiwa 2-0 ila juhudi za Miguel Baeza ziliambulia patupu baada ya kombora lake kugonga mwamba wa goli la Barcelona.

Mbali na Fatu, Bojan is the only other player to reach ndiye mwanasoka mwingine aliyewahi kufungia Barcelona mabao 10 kabla ya kutimu umri wa miaka 18.

Mabao 10 ya Fati ndani ya jezi za Barcelona yamefungwa kutokana na jumla ya mechi 26 za La Liga. Messi alihitaji michuano 30 kambini mwa Barcelona kufikisha idadi hiyo ya mabao.

Fati amepachika wavuni mabao matatu kati ya saba yanayojivunia na Barcelona hadi kufikia sasa msimu huu katika kivumbi cha La Liga. Chipukizi huyo alicheka na nyavu mara mbili katika ushindi wa 4-0 uliosajiliwa na Barcelona dhidi ya Villarreal katika mechi ya kwanza ya ligi msimu huu.

Mabao mengine ya Barcelona yametokana na wapinzani wao kujifunga mara mbili huku mengine yakifumwa wavuni kupitia Messi na Roberto.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO