DimbaMichezo

Toto la Slovakia laahidi kuwapa asali Mbappe na Griezmann wakiwika Euro 2024

Na CHRIS ADUNGO June 29th, 2024 2 min read

MWANAMITINDO raia wa Slovakia, Veronika Rajek, ameahidi kuwapa wanasoka na mashabiki wa Ufaransa burudani bomba iwapo kikosi hicho kitanyanyua Kombe la Ulaya (Euro) 2024 linaloendelea nchini Ujerumani.

Veronika, 28, ameapa kuvua nguo zote ili kuwapa masogora wa Ufaransa mshawasha zaidi wa kutamba kwenye kipute hicho baada ya kufuzu hatua ya 16-bora.

“Burudani itakuwa murua kabisa. Kylian Mbappe na Antoine Griezmann lazima waonje asali iwapo wataongoza timu yao kubeba kombe,” akasema kipusa huyo aliyenukiliwa na gazeti la SunSport.

Licha ya kwamba tzaifa lake la Slovakia pia limefuzu raundi ya 16-bora, Veronika amekuwa akijipaka rangi za bendera ya Ufaransa mashavuni, usoni na kifuani kuashiria penzi lake kwa kikosi hicho.

“Iwapo Mbappe na Griezmann wataongoza Ufaransa kutawazwa mabingwa, basi burudani itakuwa ya bure kwa kila mmoja wao kikosini. Lakini tuzo ya wawili hao itakuwa spesheli zaidi!” akasema.

Katika jaribio la kumtia Griezmann kishawishini, Veronika aliwahi kuvua nguo kuonyesha alivyochanja jina lake kwenye sehemu za ndani ya mapaja yake ili kusherehekea ufanisi wa fowadi huyo kambini mwa Atletico Madrid muhula jana.

Tukio hilo nusura lisambaratishe ndoa ya Griezmann na mkewe Erika Choperena.

“Naona Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Uhispania zikitinga nusu-fainali kisha Ufaransa wabebe Kombe,” akasisitiza.

Kipusa huyo amedokeza uwezekano wa kujitoma uwanjani akiwa tuputupu wakati wa fainali iwapo Ufaransa watatinga hatua hiyo.

Kipusa huyo amedokeza uwezekano wa kujitoma uwanjani akiwa tuputupu wakati wa fainali iwapo Ufaransa watatinga hatua hiyo. Chini ya kocha Didier Deschamps, Ufaransa watavaana na Ubelgiji katika hatua ya muondoano mnamo Jumatatu.

Katika jaribio la kumtia Griezmann kishawishini, Veronika aliwahi kuvua nguo kuonyesha jinsi alivyochanja chale za jina la sogora huyo kwenye sehemu za ndani ya mapaja yake ili kusherehekea ufanisi wa fowadi huyo kambini mwa Atletico Madrid muhula jana.

Tukio hilo nusura lisambaratishe ndoa ya Griezmann na mkewe, Erika Choperena. Erika alianza kutoka na Griezmann kimapenzi mnamo 2011 na wakafunga pingu za maisha Juni 15, 2017.

Mwanambee wao, Mia, alizaliwa mnamo Aprili 8, 2016 kabla ya mtoto wa pili, Amaro, kutua duniani mnamo Aprili 8, 2019.