Toyota Kenya kutuza mwanafunzi bora Sh500,000 katika uchoraji gari

Toyota Kenya kutuza mwanafunzi bora Sh500,000 katika uchoraji gari

Na Leonard Onyango

KAMPUNI ya magari ya Toyota Kenya, imetangaza tuzo ya Sh500,000 kwa mwanafunzi atakayeibuka mshindi wa shindano la uchoraji wa magari mwaka huu.

Kampuni hiyo jana ilisema kuwa shule ya mwanafunzi bora itatuzwa kitita cha Sh1 milioni.Wanafunzi wanaohitaji kushiriki makala ya 14 ya shindano hilo, linalojulikana kama Toyota Dream Car Art Contest, wamehitajika kutuma michoro yao kufikia Januari 31, mwaka huu.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa washindi kutuzwa kitita cha fedha. Washindi wa makala yaliyopita walipelekwa katika makao makuu ya Toyota nchini Japan.

Kulingana na Toyota Kenya, mchoro utakaowavutia waamuzi ni sharti uwe wa ubunifu na kuonyesha mwonekano wa magari katika siku za usoni.

 

You can share this post!

Wanafunzi 170,000 waliokosa kurejea shuleni wasakwa

KING’ORI: Visa vya wanafunzi kushambulia walimu...