Kimataifa

Trump ameruhusu wanawake kupapaswa sehemu nyeti, mwanamume ajitetea

October 24th, 2018 1 min read

MASHIRIKA NA PETER MBURU

MWANAMUME kutoka Florida, Marekani ambaye anatuhumiwa kumgusa sehemu za siri mwanamke walipokuwa wakisafiri kwa ndege ameeleza afisa wa FBI kuwa “Rais wa Amerika husema ni sawa kuwapapasa wanawake sehemu nyeti.”

Hii ni kulingana na malalamishi yaliyorekodiwa kuwa Bruce Michael, mwanaume wa miaka 49 na mkazi wa eneo la Tampa yuko kizuizini baada ya kukamatwa Jumapili.

Alishtakiwa na makosa ya kumshika mwanamke sehemu nyeti wakati huo wa kusafiri kutoka Houston kuelekea Albuquerque, New Mexico.

Bado haijabainika ikiwa mwanaume huyo ana wakili.

Mashtaka hayo humletea mtuhumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela na faini ya Sh2.5 milioni.

Mwanamke aliyedhulumiwa alieleza wachunguzi kuwa alihisi usingizi baada ya kuabiri ndege, lakini takriban dakika 20 baadae akaanza kuhisi mguso kwenye upande wa kulia wa sweta aliyovalia.

Alisema alihisi “nguo zikisonga na mguso wa vidole upande wa kulia na karibu na sidiria.”

Ripoti ya polisi aidha ilisema mwanamke huyo alipoangalia aliona mkono kutoka kiti cha nyuma na kudhani ni makosa

Lakini baada ya dakika 30 alihisi mguso kwenye matiti tens, mlalamishi akisema aliona mkono wenye vidole vinono vyenye nywele na kucha chafu.

Mwanamke huyo alimlalamikia mwanaume huyo aliyekuwa ameketi nyuma yake na kumwambia haikuwa sawa, kisha akahamishiwa kuketi nyuma ya ndege.

Hata hivyo, Alexander alisema kuwa alilala muda mwingi wa usafiri na alipotiwa pingu aliuliza angefungwa muda gani kwa kosa hilo.