Makala

Trump amwita Kamala Harris ‘mwanamke mrembo sana’ akimfananisha na mkewe Melania

Na WINNIE ONYANDO August 14th, 2024 1 min read

RAIS wa zamani wa Amerika Donald Trump amemrejelea mgombea urais wa Chama cha Democrat Kamala Harris kama “mwanamke mrembo sana.”

Akijadiliana na mmiliki wa mtandao wa X (zamani Twitter), bilionea Elon Musk kwenye mtandao wa kijamii ya X Space, Agosti 13, 2024, Trump alikiri kuwa Harris ni mwanamke mrembo sana na hata kumfananisha na mkewe Melania Trump.

“Kwa kweli, anafanana sana na aliyekuwa Mama Taifa Melania. Hafanani na Camilla [Malkia wa Uingereza] hata kidogo. Lakini bila shaka yeye ni mwanamke mrembo.”

Trump alisema hayo alipoulizwa kuhusu Harris alivyochapishwa kwenye jalada la jarida la Time.

Hii ni kinaya sana ikizingatiwa kuwa wote wawili wanang’ang’ania kiti hicho cha juu katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Matamshi hayo ya Trump yamezua mjadala mkali kwenye mtandao wa kijamii huku baadhi ya watu sasa wakikemea matamshi hayo

Baadhi ya watu kwenye mtandao wa kijamii wanasema kuwa Trump anafaa kujihusisha na masuala ya kisiasa na kukoma kuanza kumrejelea mpinzani wake kama ‘mwanamke mrembo’ ikifasiriwa kwamba hamchukulii kwa uzito kuhusu majukumu muhimu ya urais.

Baadhi ya maoni yaliyotolea kwenye mtandao wa X ni:

Matamshi hayo ya Trump yanajiri miezi michache tu baada ya nyota wa kurekodi video za ngono mtandaoni, Stormy Daniels, kukiri kwamba walishiriki ngono na Rais huyo wa zamani mwaka wa 2006, jambo ambalo Trump amekuwa akikana.

Daniels alikiri hayo alipofika mbele ya mahakama.

Haya yanajiri huku umaarufu wa Harris kisiasa ukiendelea kupaa hasa baada ya kumchagua Gavana wa Minnesota Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa urais wa Novemba 5, mwaka huu.