Trump sasa apanga kuzindua mtandao

Trump sasa apanga kuzindua mtandao

Na AFP

ALIYEKUWA rais wa Amerika Donald Trump ametangaza kuwa ataanzisha mtandao wake atakaotumia kuwasiliana na wafuasi wake baada ya kupigwa marufuku katika mtandao wa Twitter.

Mshauri wa Trump, Jason Miller, alisema kuwa kiongozi huyo atazindua mtandao wake wa kijamii baada ya miezi mitatu ijayo.

“Rais Trump atarejea kwenye mitandao ya kijamii ndani ya miezi mitatu ijayo,” akasema Miller.

Alisema mtandao wa kijamii wa Trump huenda ukatoa ushindani mkali kwa mitandao ya Twitter, Facebook kati ya mingineyo.

Trump alipigwa marufuku kutumia Twitter na Facebook kufuatia vurugu zilizotokea Januari ambapo wafuasi wake walivamia majengo ya Bunge jijini Washington DC.

Watu watano, akiwemo afisa wa polisi, waliangamia wakati wa vurugu hizo.

You can share this post!

Mexican Open: Kaka wawili Ken na Neal Skupski wawika

MAKALA MAALUM: Awadh hajasoma ila anasifika kwa kuongoza...