Tufani ya UDA yamsomba mkuu wa kampeni za Raila

Tufani ya UDA yamsomba mkuu wa kampeni za Raila

NA MWANGI NDIRANGU

GAVANA wa Laikipia, Ndiritu Muriithi ambaye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya kampeni ya Kinara wa Azimio la Umoja One Kenya, ni kati ya wanasiasa ambao walisombwa na mafuriko ya UDA katika eneo la Mlima Kenya.

Matokeo ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) yalionyesha kuwa, Bw Muriithi alipata kura 48,812 pekee huku Joshua Irungu wa UDA ambaye alikuwa gavana wa kwanza, akipata kura 113,380.

Katika uchaguzi wa 2017, Bw Muriithi alimbwaga Bw Irungu kama mwaniaji huru licha ya chama cha Jubilee kutwaa viti vingi eneo hilo.

Kwa muhula mmoja aliokuwa uongozini, Bw Muriithi alionekana kati ya magavana wachapakazi kutoka Ukanda wa Mlima Kenya na kote nchini.

Serikali yake iliimarisha miundomsingi na pia kuunganisha maji katika maeneo kame kwenye kaunti ndogo ya Mukogo, Laikipia Kaskazini.

Alikuwa kati ya magavana ambao waliimarisha mapato ya magatuzi yao, kwa kukusanya ushuru wa Sh1 bilioni kufikia mwishoni mwa mwaka wa kifedha wa 2021/22 mnamo Juni.

Baadhi ya wakazi waliambia Taifa Leo walimtema kwa kumuunga mkono Bw Odinga.

  • Tags

You can share this post!

Mung’aro aahidi kuing’arisha Kilifi kimaendeleo

DOUGLAS MUTUA: Kumbe wanasiasa Kenya watoshana nguvu,...

T L