Tume yatangaza nafasi elfu 14 za kazi ya ualimu

Tume yatangaza nafasi elfu 14 za kazi ya ualimu

NA DAVID MUCHUNGUH

TUME ya Kuajiri Walimu (TSC) imetangaza nafasi 14,460 za kazi ya ualimu katika shule za msingi na upili nchini.

Hatua hiyo ni katika juhudi za kupunguza uhaba mkubwa wa walimu katika shule za umma nchini.

Tume hiyo ilisema inalenga kuwajiri walimu wapya 5,000 mwezi ujao na kujaza nafasi 8,230 za walimu walioondoka kwenye taaluma hiyo kwa sababu tofauti kama vile vifo, kujiuzulu na kustaafu.

Kwenye nafasi hizo mpya, walimu 3, 972 wataajiriwa katika shule za upili huku 1,000 wakiajiriwa katika shule za msingi.

Taasisi za mafunzo ya walimu zitapokea walimu 28.

Tume hiyo pia inalenga kuwaajiri walimu katika maeneo kame kama vile kaunti za Garissa, Mandera na Wajir.

Kaunti hizo ni miongoni mwa maeneo yanayokumbwa na uhaba mkubwa zaidi wa walimu kutokana na ukosefu wa usalama.

Tangazo hilo linajiri wakati vigogo wakuu wa kisiasa wanatoa kila aina ya ahadi kuhusu mikakati watakayoweka kuajiri walimu.

Walimu hao wataajiriwa kwa mfumo wa kazi za kudumu.

Kwenye mwaka huu wa matumizi ya fedha za serikali, tume hiyo ilitengewa jumla ya Sh2.5 bilioni za kuwaajiri walimu wapya watakaopewa kazi za kudumu, na Sh1.2 bilioni za kuwaajiri walimu wengine kwa mfumo wa kandarasi.

Kijumla, tume itawaajiri walimu 6, 539 katika shule za msingi na wengine 1,691 katika shule za upili.

  • Tags

You can share this post!

Arsenal wapata kipa mpya kutoka Amerika

Wajackoyah apata mpiga debe anayemfanana

T L