Michezo

Tundo aonyeshwa kivumbi mbio za magari Mombasa

August 13th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

DEREVA Carl ‘Falsh’ Tundo ameonyeshwa kivumbi na Baldev Chager katika duru ya sita ya Mbio za Magari za Kenya (KNRC) ya KCB Mombasa Rally, Jumamosi.

Tundo, ambaye aliingia duru hii akiwa na motisha kubwa kutokana na ushindi wake katika duru tatu zilizopita za Safari Rally mwezi Machi, Athi River Rally mwezi Juni na Machakos Rally mwezi Julai, amekamilisha katika nafasi ya tatu.

Chager na mwelekezi wake Ravi Soni katika gari la aina ya Mitsubishi Evolution 10 walifuatwa katika nafasi ya pili na Onkar Rai, ambaye alishinda duru ya ufunguzi mjini Nakuru mwezi Februari, kabla ya Tundo kufunga tatu-bora. Rai na mwelekezi wake Gavin Lawrence waliendesha gari la aina ya Skoda Fabia naye Tundo na mwelekezi wake Tim Jessop wakatumia gari lao la Mitsubishi Evolution 10.

Madereva 25 walijiandikisha kushiriki mashindano, lakini Adil Mirza, Sarit Shah, Imran Khan, Akbar Khan, Edward Maina, Daren Miranda, Evans Kavisi, Ammar Haq, Frank Tundo, Piero Canobio, Aakif Virani na Jasmeet Chana hawakumaliza mashindano kutokana na matatizo mbali mbali.

Matokeo (tisa-bora):

  1. Baldev Chager/Ravi Soni (Mitsubishi Evolution 10)
  2. Onkar Rai/Gavin Lawrence (Skoda Fabia)
  3. Carl Tundo/Tim Jessop (Mitsubishi Evolution 10)
  4. Eric Bengi/Tuta Mionki (Subaru Impreza)
  5. Izhar Mirza/Kavit Dave (Mitsubishi Evolution 10)
  6. Tejveer Rai/Zahir Shah (Mitsubishi Evolution 10)
  7. Farhaaz Khan/Keith Henrie (Mitsubishi Evolution 10)
  8. Sohanjeet Puee/Adnan Din (Subaru Impreza)
  9. Nikhil Sachania/Alfir Khan (Mitsubishi Evolution 10)