Kimataifa

Tundu Lissu hatarini kuzimwa kujipigia debe kufuatia madai

September 30th, 2020 2 min read

Na THE CITIZEN

MGOMBEA wa urais wa chama cha Chadema Tundu Lissu yumo hatarini kupigwa marufuku ya kuendeleza kampeni za urais kwa muda.

Msajili wa Vyama vya Kisiasa (RPP) pamoja na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (NEC) nchini humo inataka ufafanuzi kuhusu matamshi yake aliyotoa katika kampeni zinazoendelea wiki hii.

Akijibu haraka agizo hilo, Lissu alieleza mkutano wa kisiasa mjini Musoma kwamba, afisi ya msajili wa vyama vya kisiasa inamtaka afafanue matamshi ambapo alinukuliwa akisema kwamba hawatakubali wizi wa kura safari hii.

Bw Lissu huenda akaonywa vikali, akapigwa faini au asitishwe kufanya kampeni kwa muda fulani.Bw Lissu, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa chama chake RPP, pia anadai ufafanuzi kuhusu ukusanyaji wa raia ili kulinda kura zao katika Siku ya Uchaguzi, jambo ambalo linatishia amani na usalama nchini.

‘Jibu langu kwa RPP ni kwamba, taarifa yangu inasisitiza kuwepo uchaguzi huru na wa haki ambao utaruhusu wadau kushirikishwa kulingana na maelekezo ya katiba, kanuni na sheria,’ alisema.

Kulingana naye, chaguzi huru na za haki zinapaswa kuruhusu maajenti kuapishwa, kuruhusiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura, kupatiwa vyeti vya matokeo na kutangaza washindi wote katika nyadhifa za baraza, bunge na urais.

‘Hatutakubali ikiwa maajenti wetu hawataapishwa, kukatazwa kuingia katika vituo vya kura au iwapo hawatapatiwa vyeti vya matokeo. Watu wanaohusiana na maamuzi hayo ndio watakaolaumiwa kwa matukio yatakayofanyika,’ alieleza umati uliokuwa ukimshangilia.

Alisema kuwa, Chadema imefahamu kuwa kuna mipango ya kuwaweka watu wasio wanachama kama maajenti wao ili kutatiza kura watakazopigiwa wagombea wao, akisisitiza hilo halitakubaliwa.

Mbunge huyo wa zamani eneo la Singida Mashariki na Rais wa Shirika la Sheria Tanganyika alisema, chaguzi huru zinamaanisha kuwaruhusu wapiga kura waliosajiliwa kupiga kura zao bila kutatizwa.

‘Tumefahamishwa kwamba kulikuwa na vijana walioandaliwa na CCM kusababisha vurugu katika vituo vya kupigia kura. Chama chetu kitapinga yeyote anayehusika na njama kama hizo. Chaguzi huru na za haki zinahitaji washindi kutangazwa katika chaguzi za baraza, bunge na rais,’ akasema akisisitiza kwamba hawatakubali iwapo wagombea walioshindwa hadharani watatangazwa washindi.

Alisema wanaopanga njama za kutangaza wagombea walio na kura chache kama washindi watatwikwa jukumu kuhusu chochote kitakachotokea baadaye.