Makala

TUONGEE KIUME: Kaka, miereka ya chumbani yahitaji ubunifu wa juu


MTU yeyote anaweza kufanya ngono lakini ni wachache tu wanaoweza kufanya mapenzi. Ndio, kaka umenisikia na unashangaa, huu ndio ukweli ambao watu wengi hawajui.

Naam kaka, kufanya mapenzi ni sanaa inayoanza kabla ya tendo lenyewe.

Kama hauelewi sanaa ya kufanya mapenzi, basi utajikwaa katika tendo lenyewe la kufanya mapenzi.

Sikiza, mapenzi ni suala la kiroho na ngono ni suala la kimwili. Ikiwa unadhani kufanya mapenzi ni kumvua nguo na kufanya mambo yako kwa dakika mbili au kumi na kufumukana, basi umekosea pakubwa.

Sanaa hii inaanza kwa kuandaa mtu wako kwa shughuli na inahitaji ustadi. Umenisikia tena, inahitaji ustadi.

Ukweli ni kwamba wanawake wengi wanapenda tendo la ndoa lakini wamepoteza hamu nayo kutokana na jinsi wanaume wao wanavyowachukulia kitandani.

Unambusu kwa nguvu sana, unaminya titi lake kama chungwa ambalo halina maji ndani yake, hakuna mdekezo wa kutosha kumlainisha  kabla ya tendo, hauna subira hata ya kuangalia au kujua kama amelainika kabla ya kupenya, haujali ilmradi umeridhika.

Kaka jifunze sanaa kabla ya mapenzi. Wacha ushamba.

Wacha kuzima taa, akina dada wanapenda kukutazama usoni ukiwashughulikia na makeke yako, mweleze unavyotaka akushughulikie.

Mtu wako anaridhika pale anaposema hivyo si unapofikiri hivyo.

Jifunze kumsikiza mchumba wako akueleze jinsi anavyotaka umshughulikie, usizibe masikio wakati wa kufanya mapenzi, jifunze kusikiliza lugha ya mwili wa mwenzi wako na mienendo yake, anachosema wakati wa tendo na uliza kama unafanya vizuri na uwe wazi kujifunza.

Unapofanya mapenzi na mwanamke kwa kumshirikisha kimwili, kisaikolojia na kihisia hautahangaika kumridhisha. Iguse nafsi yake, roho na mwili wake vyote vitakuwa vyako.

Kaka, ngoma yataka makeke, hainogeshwi na ukawaida, inahitaji ubunifu, inahitaji ustadi na zaidi ya yote inahitaji kujali mtu wako.

Kufanya mapenzi hakuhitaji fujo, hizo wachia wachezaji wa sinema za ngono. Kufanya mapenzi kunahitaji maelewano, sio kushurutishana.

Ukiwa mtu wa kufanya kazi nzuri, mwenzi wako atakuwa akikuhitaji umshungulikie, umpe na kumkoleza raha, umrushe roho na kufanya mwili na akili yake ichangamke.

Kuna kaka ambao huwa wanabaka wake zao wakidhani wanawapa raha kwa kufanya ngono nao wakidhani wanawashirikisha kwa mapenzi huku wakidai ni haki yao.

Ni haki ya akina dada pia kuandaliwa na kushughulikiwa vyema. Kwa hivyo kaka, wacha ubinafsi. Jifunze kufanya mapenzi badala ya kuchemkia ngono, elewa tofauti ya vitendo hivi viwili ambayo ni jinsi ya utekelezaji.

Mwenzi wako sio  mpita njia wa kuparamia kama windo. Kufanya mapenzi kunashirikisha wahusika wote wawili mili yao ikiitikiana.