Makala

TUONGEE KIUME: Ole wako ewe kaka unayemnyima mkeo joto asubuhi

Na BENSON MATHEKA June 29th, 2024 2 min read

NAOMBA kuzungumza na akina kaka walio katika ndoa ambao huwa wanaharakisha wake zao kurauka alfajiri wakawaandalie staftahi hasa wikendi.

Kaka uliye na hulka hii, unakosea. Muache mkeo afurahie joto lako alfajiri hadi kupambazuke iwapo hamuendi kazini.

Hakuna kitu kinachoridhisha mwanamke kama kupashwa joto na mumewe na kuepuka kibaridi cha mapambazuko. Huu ni ule wakati ambao wanandoa huwa wanachangamkiana sana baada ya mili yao kutulizwa na usingizi.

SOMA PIA: Mapenzi si miereka ya chumbani tu, tenga muda wa mtu wako

Ndiyo inaitwa morning glory kwa lugha ya mtaa na ole wako ewe mwanamume unayemnyima mkeo haki hii.

Unamnyima raha na usishangae wenzake huko nje wakijua na kukujadili kwa tabia zako. Hii ni kwa sababu wanawake wanapokutana kijiweni, namaanisha katika vikao vyao rasmi vya chama na visivyo rasmi kule saluni, kaka utajadiliwa.

Katika vikao hivyo, akina dada huwa wanajadili tajiriba yao chumbani na wanaojua raha ya morning glory na manufaa yake wakimpasulia mkeo, kaka utakuwa mashakani.

Hali itakayokupata itategemea na mtu wako lakini kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia ni kuwa atakununia asubuhi na utakuwa na wakati mgumu.

SOMA PIA: Kitanda kidogo ni smaku ya ndoa, mshauri wa masuala ya mapenzi asema

Haufai kusubiri kazi unayoweza kuifanya itie doa uhusiano wako na mkeo. Mpe haki yake alfajiri. Cheza kama wewe. Si ni wako, mbona umuache asononeke ilhali kazi unaweza kutekeleza.

Kulegea huku kumewafanya wanaume wengi kupata wakilea wana wasio wao (hii ni mada ya siku nyingine).

Lakini wacha leo nikupashe siri; ukitimizia mkeo haki ya dozi ya tendo la ndoa asubuhi, huwa unamuanzishia siku vyema. Hiyo dozi ya morning glory huwa inamchangamsha siku nzima na jioni ikifika, utampata akiwa tayari amekupanga upendavyo.

Hali ni kinyume na wanaowakurupusha wake zao waende kuwaandalia chai siku za wikendi ambazo huwa wanapumzika nyumbani baada ya wiki ya shughuli tele.

SOMA PIA: Kaka, kupigana au kuua kwa sababu ya mapenzi ni ujinga

Huu ndio wakati wa kukaribiana, kudekezana bila haraka. Kumbuka hiyo sio hisani ambayo huwa unamtendea mtu wako, ni haki yake unayompa mkeo na pia ana haki ya kuidai.

Kwa hivyo, ukiona mkeo akikununia asubuhi siku ya mwisho wa juma, usimlaumu, jilaumu mwenyewe kwa kushindwa na jukumu lako la kumpa haki yake na sio kwamba anajipenda, anakujali pia kwa kuwa dozi ya tendo la ndoa alfajiri inafanya mwili kusisimka na akili kuchangamka mchana wote.

Hivyo basi ukiona mwanadada akitabasamu asubuhi, mtu wake huwa amefanya kazi yake, nawe fanya yako kwa mtu wako aweze kushinda akitabasamu.

Hakuna mwanamume mwenye afya nzuri anayefaa kushindwa na morning glory ambayo wale wanaojua umuhimu wake wanasema huwa ni automatic kwa kuwa kila kiungo huwa chonjo kwa kazi yake alfajiri.

Kama unajua, unajua na kama hujui, tafuta ushauri kutoka kwa mkeo, amekujadili na kupata ushauri kule vijiweni!