TUSIJE TUKASAHAU

TUSIJE TUKASAHAU

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji jana Alhamisi alisema kuwa uchunguzi kuhusu sakata ya ufisadi, ya Sh7.8 bilioni, katika Mamlaka ya Dawa Nchini (KEMSA) ungali unaendelea na akawataka Wakenya kuwa na subira.

Lakini anafaa kukumbuka kuwa mnamo Septemba 18, 2020, Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) ilikamilisha uchunguzi wake na kuwasilisha faili kwa afisi yake.

Baadaye Bw Haji alitangaza kuwa afisi yake iliteuwa kamati ndogo ya maafisa sita kufanya uchunguzi huria wa faili hizo.

Alhamisi, Bw Haji hakusema iwapo kamati hiyo iliwasilisha ripoti kwake au la, ikizingatiwa kuwa afisi yake ilifeli kuheshimu makataa yaliyotolewa na Rais Uhuru Kenyatta kuhusu sakata hiyo.

Wakati huo, kiongozi wa taifa aliamuru kwamba uchunguzi kuhusu sakati hiyo ukamilishwe ndani ya siku 21 na wahusika wafunguliwe mashtaka.

Hadi leo, washukiwa hao, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Kemsa, Jonah Manjari, Mkurugenzi wa Ununuzi Charles Juma na mwenzake wa Idara ya Biashara Eliud Muriithi hawajafunguliwa mashtaka na wangali wanafurahia nusu ya mishahara yao baada ya kusimamishwa kazi.

You can share this post!

EACC yaahidi kuchuja vikali wawaniaji 2022

Wakulima sasa wauza mahindi yao nje ya nchi

T L