TUSIJE TUKASAHAU: Yatani asije akasahau kuwa wakazi wa Marsabit na maeneo mengine ya Kaskazini Mashariki, bado wanakeketwa na njaa

TUSIJE TUKASAHAU: Yatani asije akasahau kuwa wakazi wa Marsabit na maeneo mengine ya Kaskazini Mashariki, bado wanakeketwa na njaa

MAELFU ya wananchi bado wanaathirika kwa njaa katika Kaunti ya Marsabit kutokana na hali ya ukame inayoshuhudiwa katika eneo hilo ilivyoripotiwa katika gazeti la Taifa Leo, Jumatatu.

Hii ni licha ya kwamba mnamo Septemba 8, 2021 Rais Uhuru Kenyatta alitangaza ukame kuwa janga la kitaifa na kuelezea kujitolea kwa serikali kuweka mikakati ya kudhibiti changamoto hiyo.Hii ndio maana akihutubu katika sherehe ya Mashujaa Dei, Kaunti ya Kirinyaga, Rais Kenyatta aliamuru Hazina ya Kitaifa kutenga Sh2 bilioni za kufadhili mipango kupunguza makali hayo.

Lakini Waziri wa Fedha Ukur Yatani asije akasahau kuwa wakazi wa Marsabit na maeneo mengine ya Kaskazini Mashariki, bado wanakeketwa na njaa, ukosefu wa maji huku mifugo na watu wakifa.

Mnamo Novemba 6, wabunge wakiongozwa na Aden Duale (Garissa) walimtaka Bw Yatani afike mbele ya kamati ya fedha aelezee jinsi fedha hizo zilivyotumika, lakini mpaka sasa hajafika.

You can share this post!

Tangatanga wavuruga hoja ya kuunda kamati ya bajeti

UJASIRIAMALI: Ameunda jina kuwa bingwa wa asali ‘legit’

T L