TUSIJE TUKASAHAU: Badi asije akasahau kuwa karibu hospitali sita mpya zilizojengwa chini ya usimamizi wake hazina dawa na vifaa vingine vya matibabu

TUSIJE TUKASAHAU: Badi asije akasahau kuwa karibu hospitali sita mpya zilizojengwa chini ya usimamizi wake hazina dawa na vifaa vingine vya matibabu

MNAMO Februari 2020 Shirika la Huduma za Jiji la Nairobi (NMS) lilianza kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali 19 katika mitaa mbalimbali ya mabanda jijini kwa ufadhili wa Serikali Kuu.

Hospitali hizo mpya zilinuiwa kutoa huduma za afya kwa mamilioni ya wakazi wa vitongoji hivi duni, bila malipo, na hivyo kupunguza misongamano katika hospitali za; Mama Lucy Kibaki, Mbagathi na Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Lakini Luteni Jenerali Mohamed Badi asije akasahau kuwa karibu hospitali sita mpya zilizojengwa chini ya usimamizi wake, na kuzinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta, na kuzinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta hazina dawa na vifaa vingine vya matibabu.

Wakazi wanaofululiza kila siku katika hospitali hizo, za viwango vya Level 2 na Level 3, hukosa huduma na kulazimika kusaka huduma hizo katika hospitali za kibinafsi kwa gharama wasioweza kumudu.

  • Tags

You can share this post!

Shirika latilia shaka maandalizi ya IEBC

Ndoa ya Mudavadi, Ruto yachanganya wawaniaji Magharibi

T L