TUSIJE TUKASAHAU: Chokoraa wangali tishio jijini

TUSIJE TUKASAHAU: Chokoraa wangali tishio jijini

VIJANA wanaorandaranda mitaa, maarufu kama chokoraa, wangali tishio la usalama katika barabara kadha katikati mwa jiji la Nairobi.

Visa vya watu, haswa wanawake, kuhangaishwa na hata kupokonywa mikoba na vijana hawa hutoa mara kadhaa haswa katika barabara zenye shughuli nyingi kama zile za Tom Mboya Road, Kirinyaga Road na River Road.

Lakini safu hii inamkumbusha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Huduma za Jiji (NMS) Luteni Jenerali Mohamed Badi kwamba mnamo Februari 25, 2019 aliahidi kuondoa kuondoa kero la chokoraa jiji.

Aliahidi kuanzisha mpango wa kuwaondoa vijana hao barabarani na kuwapeleka katika vituo vya kurekebisha tabia ili wapewe mafunzo mbalimbali ya kuwasaidia maishani.

Vituo hivyo ni kama vile Bahati Reception Centre, Pumwani Reception Centre, Joseph Kangethe Reception Centre na hata Shirika la Vijana kwa Huduma za Taifa (NYS).

Muda wa kuhudumu kwa NMS ukitarajiwa kukamilika Agosti 2022, Jenerali Badi asije akasahau kutimiza ahadi yake ya kuondoa chokoraa na familia za barabarani jijini Nairobi na viungani.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Unafiki mkubwa kwa Kenta, Khalwale kuvumisha...

Nitafurusha jeshi la Uganda kutoka Migingo – Raila

T L