TUSIJE TUKASAHAU: Dkt Alfred Mutua asije akasahau aliahidi kuzikabarati sanamu

TUSIJE TUKASAHAU: Dkt Alfred Mutua asije akasahau aliahidi kuzikabarati sanamu

MNAMO Juni 26, 2019 Gavana wa Machakos Alfred Mutua aliahidi kukarabati na kutunza sanamu za mashujaa wa ukombozi wa taifa hili Tom Mboya na Dedan Kimathi zilizoko katikati mwa jiji la Nairobi.

Alisema ni aibu kwamba sanamu hizo zimetelekezwa na kuwa katika hali mbaya ilhali Mboya na Kimathi ni mashujaa waliopigania ukombozi wa taifa hili.

“Nimegadhabishwa na hali mbaye ya sanamu hizi. Binafsi nitajitwika wajibu wa kuzifanyia ukarabati hadi wale wanaohusika na kazi hiyo watakapoamka kutoka usingizi wa pono,” Dkt Mutua akasema.

Lakini Gavana huyo hajatimiza ahadi hiyo miaka minne baadaye ilhali sanamu hizo ziko katika hali isiyo ya kupendeza machoni pa Wakenya na wageni.

Dkt Mutua asije akasahau kuwa aliahidi kuzikabarati sanamu hizo na hana budi kutimiza ahadi hiyo kabla ya kukamilisha muda wake wa kuhudumu kama gavana.

You can share this post!

Kizaazaa Old Trafford Man Utd ikivizia Spurs

Sevilla yadidimiza matumaini ya West Ham kupiga hatua zaidi...

T L